leseni ya biashara

Jinsi ya kupata leseni ya biashara

Leseni ya biashara hutolewa kwa makampuni na wafanyabiashara kwa ajili ya kuwapa uhalali wa kufanya biashara husika katika eneo husika na au katika sekta husika.

Leseni ya eneo: Hii ni aina ya leseni ambayo biashara zote zinatakiwa kuwa nayo. Leseni hii inatolewa na halmashauri  ya jiji, manispaa au wilaya biashara inapotegemewa kufanyikia.

Leseni ya udhibiti: Baadhi ya sekta hutoa leseni ya udhibiti wa biashara. Mfano huduma za afya, mawasiliano, utalii, elimu nk wanawataka kufanya biashara husika wanatakiwa na sheria kuomba leseni ya udhibiti wa biashara wanazotegemea kuanza kuzifanya kabla hawajafanya.

Ukishakamilisha usajili wa jina la biashara au kampuni BRELA kinachofuata ni kupata leseni ya biashara

Taratibu za kufuata ili kupata leseni ni hizi hapa chini:

Leseni zote ziwe za udhibiti (regulatory license) au ile ya eneo la kufanyia biashara hutolewa baada ya kufanya malipo ya awali ya kodi. Kwa mashirika, makampuni ni baada ya kulipa provisional tax lakini kwa watu binafsi wanapewa leseni baada ya kulipa kodi waliyokadiriwa na mtaalamu kutoka TRA.

  1. Pata kwanza TIN: TRA watakupa TIN (siku hizi unaweza kuipata TIN kwenye internet bila hata ya kwenda TRA) jisajili hapa ili kupata TIN
  2. Makadirio ya kodi: TRA wakishakupa makadirio au provisional tax unaweza kulipa benki kwenye akaunti ya Kamishna wa kodi Tanzania  au ukalipa kwa mitandao ya simu. Tafadhali tembelea website ya TRA kwa maelezo zaidi
  3. Tax Clearance: Baada ya kukamilisha malipo ya kodi inayotakiwa kisheria, TRA watakupa Tax Clearance Certificate ambayo utaitumia kwenye maombi ya leseni husika
  4. Maombi ya leseni ya eneo: Maombi ya leseni ya eneo la kufanyia biashara hufanywa kupitia fomu maalumu ambayo hupatikana kwenye ofisi za halmashauri
  5. Maombi ya leseni ya udhibiti: Maombi ya leseni za udhibiti (regulatory license) hufanyika kwa kujaza fomu maalumu zinazopatikana kwenye ofisi za udhibiti, kama biashara ni ya mawasiliano, utapata fomu TCRA, kama ni za afya utapa kwa bwana afya wa wilaya au wizara ya afya. kama ni ya utalii fomu ya maombi ya leseni ya utalii (TALA) utaipata kwenye ofisi za TTB (Tanzania Tourists Board) iliyo karibu na wewe, kama ni chuo cha VETA, hutolewa ofosi za VETA karibu na wewe, kama ni chuo cha diploma hutolewa na NACTE, kama ni chuo kikuu hutolewa na TCU, orodha inaendelea NK.

Kumbuka:

  • Tafadhali wasiliana na mshauri au mtaalamu wa sekta husika ili update maelezo ya leseni zipi zinatakiwa na utaratibu wa kuzipata ukoje.
  •  Leseni nyingi hufanywa upya (license renewal) kila mwaka, chache miaka mitatu NK

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi