Mpango Kazi ni maelezo ya namna utakavyofanya kazi kwa mtiririko na utaratibu utakaoleta tija tarajiwa. Kiingereza wanaita Action Plan au Plan of Action.
Mpango Kazi unajumuisha LENGO KUU na Malengo madogo madogo halafu Kazi zitakazofanyika (activities) ili kufikia hayo malengo madogo mpaka lile Lengo Kuu. Pia inaonyesha mhusika wa kila kazi, muda wa kufanya (hasa kuanza na mwisho wake), Mbinu za kutumia, Hatua iliyofikiwa (monitoring) Mambo mazuri yaliyojitokeza, Changamoto zilizojitokeza na n jia ya kutokea. Mwisho Tadhmini ya Mpango Kazi wote na kuweka mapendekezo ya maboresho kwa wakati ujao
Mpango Kazi unaadhiriwa ngazi ya taaluma na sekta husika
Mfano
- Mwalimu na Mwalimu mkuu au afisa wa elimu au Waziri wa Elimu
- Uhandisi au Ualimu au Sheria au Utabibu nk
Mambo muhimu katika mpango kazi
- Lengo Kuu
- Malengo mahususi
- Ratiba ya Utekelezaji
- Mambo mazuri yaliyojitokeza
- Changamoto na utatuzi wake
- Tathmini na maboresho yake
Mfano wa Ratiba ya Utekelezaji
Na | Tarehe | Kazi | Mhusika | Hali Halisi | Mbinu zitakazotumika | Maelezo Mengine | |
Kuanza | Mwisho | ||||||
1. | 12/01/2019 | 19/01/2019 | Kuitisha kikao cha Bodi | MD | Bado | Kutuma email, kupiga sim una kutumia group ya Whatsapp | Hakuna |
2. | 20/01/2019 | 29/01/2019 | Kuandika Ripoti ya Kikao cha Bodi | Afisa Tawala | Bado | Kutumia dondoo za kiako na secretarieti ya uandishi wa dondoo |
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |