Gitaa na Uimbaji Bora

Mwongozo wa Uimbaji Bora na Kuwa Wanamuziki Mwenye Mafanikio

Utangulizi

Uimbaji ni sanaa na hivyo inahitaji utaalamu, ubunifu na umahiri katika kuifanya. Unashauriwa kama ni mara yako ya kwanza kutoa album au wimbo usitoe wa video mpaka hiyo album ya audio ikubalike. Kama audio haijakubalika ni dhahiri pia na video utakayotoa haitakubalika. Hapa utakuwa umeokoa gharama zisizo za lazima. Pia unashauriwa usirekodi nyimbo nyingi kama ni mara yako ya kwanza. Utakuwa umeokoa gharama nyingi sana ya kurekodi album nzima ambayo haitapenya kwenye soko. Wimbo wako wa majaribio ukipendwa na watu wengi sasa utakuwa na ujasiri wa kuingia gharama kurekodi album ambayo hata kama nyimbo zingine ni za kawaida ile moja iliyofanikiwa itausa album nzima. Japo sishauri hivyo, kila wimbo uwe na mvuto wa kipekee.

Hatua kuu tatu (3)

Kuna hatua kuu 3 za kuyatekeleza ili uwe mwimbaji aliyefanikiwa

  1. Maandalizi ya kuimba
  2. Uimbaji wenyewe
  3. Baada ya kuimba

Maandalizi ya kuimba

Katika hatua hii ya maandalizi hakikisha mambo haya yanawekwa sawa

  1. Waimbaji wenzako
  2. Backup and background singers
  3. Vyombo vikuu
  4. Backup and Background instruments
  5. Vifaa vya muziki kama vitatoka kwako au studio (zikitoka studio unatakiwa uvijaribishe kama zinafikia kiwango unayotaka)
  6. Afya yako nk

Haijalishi unafanya mazoezi au unaimba rasmi, unatakiwa kuijua sauti yako kuwa iko fit kwenye kuimba. Kama haiku fit muone mtaalamu wa masuala ya sauti atakushauri nini cha kufanya. Pia unatakiwa kujua eneo ambalo utaimbia, kama ni studio, kanisani, jukwaani, kwenye ukumbi nk. Unatakiwa pia kufahamu vyombo utakazozitumia kama microphone, stand yake, je mic iko sensitive kiasi gani, mic ambayo ni sensitive sana haitakiwi usogeze karibu na mdomo, mikono yako, nguo zako na saa nyingine mate na pumzi yako zinaweza kutengeneza vibration ambayo itaharibu sauti lengwa. Pia unatakiwa kufanya rehearsal na wapiga vyombo na backup wote ili muwe kitu kimoja msipishane kwenye stage

Uimbaji wenyewe

Kwenye uimbaji kuna mambo makuu matano (5)

  1. Ustadi (Professionalism)
  2. Ubunifu (Innovation and Creativity)
  3. Kujiamini na kujihemsha (Confidence and self inspirational)
  4. Kumiliki jukwaa (Stage control)
  5. Kuwamiliki wafuasi au wasikilizaji au watizamaji (Audience control)

Ustadi

Wewe kama muimbaji ni lazima ufahamu taaluma ya muziki na miiko yake. Mifumo ya notes na maboresho yake. Nyimbo huwa ni mashairi, kwa hiyo ustadi kwenye kupangilia maneno na sauti ni muhimu kuliko kifani. Backup ya waimbaji, wacheza show au drama ni muhimu ipangiliwe kwa ustadi ambao utainua hisia za mashabiki na sio kuwachosha

Ubunifu

Kwenye muziki huwezi kupenyeza kwenye soko ukija na uimbaji wa kawaida hata kama unaimba vizuri. Uhalisia wako na vionjo vyako binafsi ambazo hazifanani na za wengine ni muhimu uziheshimu na kuzikuza daima. Hata kama unaimba vizuri kama Maiko Jackson, hutaweza kupenya hata 0.0000001% ya soko la Michael Jackson (Marehemu)

Washabiki, wasikilizaji na watiuzamaji wa musiki daima huwa wanatafuta kitu kipya, kiingereza wanaita “New innovations and creativity” Kama huniamini wewe wafuatilie tu waimbaji wa zamani na wapya wanaovuma kwenye sekta ya muziki, utkuta ni kwa sababu waliingia kwa staili mpya, unique na yenye kubeba uhalisia wa mtu binafsi.

Christina Shusho kaja na uimbaji wake personal style, Bahati Bukuku naye hivyo hivyo, na wengineo

Kujiamini

Silaha ya ushindi daima ni kujiamini, ukijiamini itakusaidia kutumia kwa ukubwa wake kipaji ulisho nacho na pia stadi pamoja na ubunifu ambao huwa unapotea kama wewe ni mwoga.

Kujiamini kunaimarishwa siku zote kwa kufanya mazoezi nyingi na za kila hali na maeneo. Imba ukiwa mwenyewe, ukiwa na mwenzako, ukiwa kwenye kundi, ukiwa kanisani na saa nyingine fanya matamsha na concert za bure ili kujenga kujiamini.

Ukiogopa kuimba mbele ya mtu mmoja pia utaogopa kuimba mbele ya wengi. Ukidhubutu kuimba vizuri na kwa kujiamini mbele ya mtu mmoja, pia utaweza kuimba hivyo hivyo na hata zaidi mbele ya kadamnasi.

Imba pia kwa hisia, hisia mara nyingi huoindoa woga na kumfanya mwimbaji asijitambue kama yuko mbele ya watu na hivyo kukupa fursa ya kuimba bila woga

Kumiliki jukwaa

Kumiliki jukwa ni tunda la kujiamini, kuwa mbunifu na kuimba kwa ustadi. Mtu anayemiliki jukwaa anawapagaiza watu na hivyo kuwa chanzo kikuu cha kuwafanya mashabiki wako wasichoke na kukufuatilia kwa mhemko na hisia kali ambazo ndizo siri ya kufaniukiwa kwako

Ili uweze kumiliki jukwaa ni lazima kwanza ulifahamu jukwaa, ramani yake, vitu vilivyomo, mpangfilio wa spika, kamera, backup vocal, wapiga vyombo, mashabiki wako. Mpiga solo akufuate bial shida, mpiga drums naye asipate shida kukujua uko kwenye bits za mfumo upi, mpiga gitaa za besi na zinginezo pamoja na vyombo vingine vya sauti kama keyboard wakujue uko kwenye kodi zipi ili wote wakufuate. Hata mashabiki na wao wahemke bila kupoteza bits na hisia.

Kuwamiliki mashabiki (Audience control)

Mpaka hapa utakuwa umewamiliki mashabiki wako kwa sehemu kubwa lakini bado kidogo. Utunzi wa nyimbo unaweza toa nafasi kubwa au ndgo kwa mwimbaji kuwamilki mashabiki. Hakikisha kwenye kibwagizo au ubeti wa mwisho kuna aya za mashairi zitakazokuunganisha wewe na mashabiki wako –Audince

Shairi hizo ni zile zitakazowafanya aidha wajibu, wapige makofi, wacheze au washangilie kwa kuongozwa au kivyao.

Baada ya uimbaji

Ukiisha imba wape watu mbali mbali rasimu ya wimbo au album ili wakaisahihishe na uwaambie rasmi kwamba unawataka wakukosoe na waikosoe wimbo au nyimbo ulizowapa ili wafanye hivyo vinginevyo wengi watanyamaza. Angalia utoe rasimu hiyo kwa watu wenye ujuzi tofauti. Wengine ni wa sauti, vyombo nk

Tumia maoni yao kure-produce wimbo husika au album kwa kuyarekebisha makosa yaliyogunduliwa. Ikisha toka rasimu ya mwisho kama umeimba kwa mara ya kwanza, sambaza bure kwenye TV, radio na kwenye blog, Yutube.com, Vimeo.com ili kupata sasa maoni ya wadau wenyewe ambao ni wasikilizaji, watizamaji na mashabi wako

Hutaweza kureproduce hiyo album au wimbo lakini itakusaidia sana kwenye matoleo mengine yajayo ili uyarekebishe yale madhaifu ya jumla yaliyojitokeza kwenye huo wimbo wa kwanza.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi