Kufuatilia mradi-biashara

Jinsi ya Kubuni Biashara, Kubuni Miradi

Jinsi ya Kubuni Biashara na jinsi ya Kubuni Miradi ni kitu kimoja kwa maelezo haya chini

Tafsiri

Biashara: ni mradi uliobuniwa ili kutatua matatizo au mahitaji ya watu (ambao ndio wateja) kwa malipo au fidia yenye faida

Mradi: ni kazi iliyobuniwa na kutekelezwa ndani ya muda fulani ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa

Kwa maana ya hii ya BIASHARA ni mradi uliobuniwa ili kutatua matatizo ya watu kwa malipo yenye faida ni lazima mtu anayebuni biashara kuzingatia yafuatayo:

  1. Kufanya utafiti wa matatizo yanayowakabili watu kwenye eneo lengwa
  2. Kuyachanganua hayo matatizo
  3. Kuyapanga kwa ukubwa wa tatizo
  4. Weka kipaumbele ya matatizo kama 3 hivi ambayoutakayoyashughulikia
  5. Kuyapatia ufumbuzi kila tatizo – buni shughuli/mradi ya kufanya ili kuondoa tatizo
  6. Weka mpango wa utekelezaji wa tatizo – Business Plan
  7. Weka jinsi ya kufuatilia kama tatizo liemeisha

Kufanya utafiti wa matatizo yanayowakabili watu kwenye eneo lengwa

  • Utafiti ulenge katika kutambua orodha ya matatizo yaliyopo kwenye jamii husika

Kuyachanganua hayo matatizo

  • Ingia kwenye mjadala wa kubaini kila tatizo lilisababishwa na  nini?

Kuyapanga kwa ukubwa wa tatizo

  • Panga kuanzia tatizo lenye madhara makubwa mpaka lile lenye madhara kidogo kwenye jamii

Weka kipaumbele ya matatizo kama 3 hivi ambayoutakayoyashughulikia

  • Hutaweza kwa vyovyote kushughulikia matatizo yote na kwa mantiki hii ni lazima uchukue matatizo ambayo yakishughulikiwa itaondo kundi kubwa la matatizo madogo madogo. Matatizo yasiyozidi matatu ni muafaka kabisa

Kuyapatia ufumbuzi kila tatizo – buni shughuli/mradi ya kufanya ili kuondoa tatizo

  • Kwa uzoefu wako na kwa ushauri wa kitaalamu, weka majibu ya kila tatizo katika yale  matatu uliyochagua

Weka mpango wa utekelezaji wa tatizo – Business Plan

  • Hapa ndio sehemu ya kuweka mpango madhubuti wa kutekeleza yale majibu ya kila tatizo kwa kutengeneza Mpango wa Biashara ambao utakuwa kama dira ya kuongozi utekelezaji wote wa kuyatatua hayo matatizo kwa faida

Weka jinsi ya kufuatilia kama tatizo liemeisha

  • Weka viashiria (indicators) vitakavyotumika kujua kama tatizo limeisha kwa kiasi gani

Yanayofanana:

Usimamizi wa Miradi – Wikipedia, kamusi elezo huru
http://sw.wikipedia.org/wiki/Usimamizi_wa_Miradi
Asili ya miradi kuwa ya muda mfupi ni kinyume na biashara ya kawaida (au …. inaelezea taratibu za kuratibu watu na shughuli katika mradi, jinsi ya kubuni na

Kitabu Cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri
http://www.squidoo.com/kitabu-mbinu-za-biashara
Mtunzi wa Kitabu hiki Charles P. M. Nazi ni mshauri wa masuala ya biashara. Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza

Web design na maendeleo katika Worthing, West Sussex
http://www.sw.haydendigital.com/
Hayden Digital ni kampuni ya maendeleo ya mtandao – kutoa huduma A mtaalamu internet maendeleo na ushauri wa kubuni, kuwahudumia wateja Tunatarajia kuwa na furaha na kuzungumza kwa njia ya jinsi ya kusaidia biashara yako.

Wajasiriamali wadogo waonyeshwa njia ya mafanikio – Biashara …
http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1687028/-/xm04c7/-/index.html
siku 6 zilizopita “Vijana watapatiwa mafunzo hayo baada ya wao kubuni wazo la sasa watatambua nini maana ya ujasiriamali na jinsi ya kufanya biashara.

Mbunge awapa neno wanawake
http://mtanzania.co.tz/index.php%3Foption%3Dcom_content%26view%3Darticle%26id%3D4888:mbunge-awapa-neno-wanawake%26catid%3D10:nyanda-za-juu-kusini%26Itemid%3D59
26 Des 2012 Alitoa semina ya ujasiriamali kwa wanawake na jinsi ya kubuni biashara mpya na siyo kusubiri fedha za matumizi kutoka kwa waume zao.

F. A. Hayek’s, “The Use of Knowledge in Society” | AfricanLiberty.org
http://www.africanliberty.org/content/f-hayek%25E2%2580%2599s-use-knowledge-society
Badala yake ni tatizo la jinsi ya kupata matumizi bora zaidi ya raslimali matatizo makuu ya sera ya kiuchumi – au ya kubuni mfumo wa uchumi wenye ufanisi. wa kuelekea kwenye biashara kwa ujumla, ikilinganishwa na ule wa uzalishaji.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi