Register
A password will be e-mailed to you.

hatua muhimu katika kuanzisha biasharaHatua ya ya 1: Kuamua kuingia katika biashara

Kuamua kuingia katika biashara ni majumuisho ya utayari wa kisaikolojia, kiakili, kiuchumi na kukabiliana na hatari au vitisho vyote vitakavyojitokeza kwenye biashara

Hatua ya 2: Kuchanganua uwezo na udhaifu wako

Maeneo manne ni muhimu yapatiwe taarifa halisi na kuchukua hatua ili uweze kumudu kufanya biashara husika

Mazingira wezeshi

(Mambo yanayofanya biashara ikue na kusimama)

Mazingira pingamizi

(Mambo yanayofanya biashara idumae na kufa)

Mazingira ya Ndani

(Mambo yaliyo ndani ya uwezo wa mhusika)

UWEZO

Uwezo wako katika kuendesha biashara mfano: utaalam, vitendea kazi, rasilimali kama kiwanja nk.

UDHAIFU

Udhaifu wako katika kuendesha biashara mfano: ukosefu wa utaalam, ukosefu wa vitendea kazi, ukosefu wa rasilimali kama kiwanja nk.

Mazingira ya Nje

(Mambo yaliyo nje  ya uwezo wa mhusika)

FURSA

Kuwepo kwa sera nzuri za nchi, kuwepo kwa katiba nzuri ya nchi, hali ya hewa nzuri, kuwepo mwitikio wa jamii kwenye biashara yako nk

VITISHO

Kutokuwepo kwa sera nzuri za nchi, kutokuwepo kwa katiba nzuri ya nchi, kutokuwepo kwa hali ya hewa nzuri, kutokuwepo kwa mwitikio wa jamii kwenye biashara yako nk

Hatua ya 3: Kupata mafunzo

Baada ya kujua udhaifu wako, pata mafunzo

Mfano:-        Ya kupata mafunzo ya kiufundi katika biashara husika na au ya ya kubadili mitizamo,

Hatua ya 4: Kupeleleza mazingira utakayofanya biasha ili kujua:

i)             Fursa nzuri zilizopo

ii)            Vitisho au hatari zitakazoikabili biashara yako (vihatarishi vya biashara husika kama vile sera mbovu, barabara mbovu, hali ya hewa mbovu nk)

 

Hatua ya 5: Kuchagua biashara gani ufanye

i)             Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)

ii)            Kuuza bidhaa (Trading)

iii)          Kutoa huduma (Service)

Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)

Kutengeneza bidhaa ni kutumia rasilimali watu na malighafi ili kutengeneza bidhaa ya kuuza kwa mlaji au mchuuzi. Bidhaa ni kama vyakula, vyombo, nk

Kuuza bidhaa (Trading)

Kuchuuza bidhaa zilizotengenezwa hapo juu no. A(a)

Kutoa huduma (Service)

Kutumia ujuzi wako au wa wengine katika kuwahudumia watu na shida zao kwa malipo. Mfano kufundisha, kutibu, kusafirisha, kutumbuiza nk

Hatua ya 6: Utafiti wa soko (Market Survey)

i)    Washiriki wenza wa biashara katika soko

ii)   Ukubwa wa soko

iii)   Mgawanyo wa soko kati ya washiriki

iv)    Aina ya soko/masoko

v)    Tabia ya soko NK.

English Form

Fomu ya Kiswahili


Leave a Reply

Your email address will not be published.

1 × five =

Service Quotation Request Form

Please fill the necessary information below

PO Box 1999, city, country

Fomu ya maombi ya huduma

Tafadhali jaza taarifa muhimu hapa chini

SLP 1999, mji, nchi