Register
A password will be e-mailed to you.

hatua muhimu katika kuanzisha biashara

Hatua ya 7: Kuamua aina ya mfumo wa biashara utakayofanya

Fuatilia maelezo ya kila mfumo ukitilia maanani faida na hasara za kila mfumo. Unaweza pia kumtumia mshauri wa masuala ya biashara kukushauri kulingana na mazingira yako utakayofanyia biashara.

Hasa unatakiwa kujua zaidi mambo ya kisheria katika mfumo utakaoamua kuutumia kuendesha baishara yako ili isije ikakuletea shida huko mbeleni, maamuzi ya mfumo upi uuchukue inategemea zaidi sheria za ndani ya nchi husika, pia inategemea ukubwa wa mtaji wako nk.

Mtu mmoja (sole proprietor)

Hii ni biashara inayoendeshwa na mtu mmoja tu kwa kutumia jina lake binafsi au kusajili brela jina la biashara tofauti na jina lake binafsi

Faida yake

 • Kuanzisha ni rahisi
 • Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu

Hasara yake

 • Biashara ikipata shida mmiliki anahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
 • Yaani biashara ikidaiwa mali za mmiliki kama nyumba, gari, shamba zitauzwa ili kulipa madeni

Ushirika au Partnership (watu wawili kwenda juu)

Hii ni biashara inayoendeshwa na watu wawili au zaidi kwa mfumo ule ule wa mtu mmoja lakini hapa ni lazima kusajili jina la biashara brela na kuandika mkataba wa ushirika yaani Partnership Agreement

Faida yake

 • Kuanzisha ni rahisi
 • Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu

Hasara yake

 • Biashara ikipata shida wamiliki wanahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
 • Mikataba inayoingiwa na mmoja wa washirika huwabana na wengine wasiohusika

Kampuni ya umma (public companies)(zaidi ya watu wawili bila kikomo)

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
 • Ni rahisi kuvutia mitaji mikubwa kupitia masoko ya hisa

Hasara yake

 • Haina usiri hivyo ni hatari kwani washindani wa biashara husika wanaweza kutumia taarifa hizo kujipanga
 • Muda na rasilimali muda kupotea kwa shughuli za kihasibu na kazi za makaratasi

Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa hisa

(private companies limited by shares) (watu wawili hadi 50)

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
 • Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
 • Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma

Hasara yake

 • Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
 • Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
 • Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
 • Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa udhamini

(private companies limited by guarantees) (watu wawili hadi 50)

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
 • Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
 • Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma

Hasara yake

 • Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
 • Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
 • Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
 • Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

Jumuiya (association)

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Inavutia wahisani
 • Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake

 • Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
 • Ugomvi wa mara kwa mara
 • Haina kinga kwa waazilishi

Vyama vya ushirika

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Inavutia wahisani
 • Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake

 • Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
 • Ugomvi wa mara kwa mara
 • Haina kinga kwa waazilishi

Mashirika yasiyo ya kiserikali

Faida yake

 • Utambulisho wa kisheria
 • Inavutia wahisani
 • Ni ya watu wachache waliokubaliana

Hasara yake

 • Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
 • Ugomvi wa mara kwa mara
 • Haina kinga kwa waazilishi

Ukishachagua mfumo mzuri wa biashara yako, unatakiwa kuanza mchakato wa kuisajili biashara yako katika mamlaka ya usajili wa makampuni inayoitwa BRELA ambayo ofisi zake zipo Jengo la shirika –Dar es salaam kama umeamua kutumia mifumo ya sole proprietor, partnership au makampuni. Mifumo mingine husajiliwa katika wizara husika au kwenye serikali za mitaa

English Form

Fomu ya Kiswahili


Leave a Reply

Your email address will not be published.

four × 5 =

Service Quotation Request Form

Please fill the necessary information below

PO Box 1999, city, country

Fomu ya maombi ya huduma

Tafadhali jaza taarifa muhimu hapa chini

SLP 1999, mji, nchi