Register

eleven + 5 =

A password will be e-mailed to you.

Ifuatayo hapa chini ni mfano wa uandishi wa dondoo za mkutano au kikao chochote. Maoni ya namna ya kuboresha yanakaribishwa

 

Tumaini Development Group

SLP 12908, Arusha

Taarifa ya Mkutano wa 5 wa Kikundi cha Tumaini uliofanyika Arusha Hall Tarehe 12/4/2012

Waliohudhuria

 1. Juma Hamad
 2. Mary John
 3. Kyuga Mwasige

Walioalikwa

 1. Lemayani Loitore – Mwanasheria

Wasiohudhuria

 1. Henry Mambo – Ametoa sababu
 2. Jaffar Haji

Ajenda

 1. Kufungua mkutano
 2. Kuthibitisha dondoo za mutano uliopita
 3. Kujadili yatokanayo na mkutano uliopita
 4. Mkopo wa CRDB
 5. Mkatabawa mradi wa maji
 6. Mikopo kwa wanachama
 7. Mengineyo
 8. Tarehe ya mkutano ujao
 9. Kufunga mkutano

Ajenda zilizodhibitishwa

 1. Opening of the meeting
 2. Kufungua mkutano
 3. Kuthibitisha dondoo za mutano uliopita
 4. Kujadili yatokanayo na mkutano uliopita
 5. Mkopo wa CRDB
 6. Mkatabawa mradi wa maji
 7. Mikopo kwa wanachama
 8. Mengineyo
  1. Kupokea wanachama wapya
 9. Tarehe ya mkutano ujao
 10. Kufunga mkutano

MT5-1: Kufungua mkutano

Mkutano ulifunguliwa tarehe 12/4/2012 saa 4:20 asubuhi na mwenyekiti

MT5-2: Kusoma na kuthibitisha dondoo za mkutano uliopita

Dondoo za mkutano wa nne zilisomwa na kuthibitishwa na wajumbe

MT5-3: Yatokanayo

Yafuatayo ni yatokanayo na mkutano uliopita, Maelezo zaidi kiambatanisho na. 1

 1. Katiba ya TDG

Imeazimiwa kwamba kamati ay katiba inayoongozwa na Lesom iwakilkishe rasimu ya katiba kwenye mkutano ujao

 1. Taarifa za fedha

Mkutano umeazimia kuwa marekebisho yote yaliyopendekezwa yafanyiwe kazi kabla ya mkutano ujao

MT5-4: Mkopo wa CRDB

Mkutano umeazimia kuwa Mtunza hazina na wajumbe wawili wa mkutano wafuatilie na kujaza fomu za mkopo na kuwakilisha kwa mwenyekiti kwa ajili ya kuchukuliwa maamuzi kwenye mkutano ujao

MT5-9: Mkataba wa mradi wa maji

Kamati ndogo ya maji imepewa kazi ya kuusoma mkataba wa mradi wa maji kwa kushirikiana na mwanasheria na kuleta ripoti kwenye mkutano ujao

MT5-10: Mikopo kwa wanachama

Imeazimiwa kuwa wanachama wanaotaka mkopo wa kujen ga nyumba na wanakidhi masharti yote wapewe mikopo bila kuzungushwa

MT5-11: Mengineyo

 1. Kupokea wanachama wapya

Mkutano umeazimia kuwa zoezi la kuwaingiza wanachama wapya lisimamishwe mpaka hapo mkutano kama huu utakapotoa maamuzi mwengine

ES4-12: Tarehe ya mkutano ujao

Mkutano umeweka tarehe 15/5/2012 saa 4.00 asubuhi kuwa ndio tarehe na sa ya mkutano ujao utakaofanyika Arusha Hall

ES4-13: Kufunga mkutano

Mkutano ulifungwa na mwenyekiti tarehe 12 Aprili 2012 saa 11 Jioni

 

Im esainiwa na:

 

Mwenyekiti Katibu

[dm]30[/dm]

English Form

Fomu ya Kiswahili


About The Author

Lemburis Kivuyo is a Busi­ness, IT and Com­mu­nity Related Project Consultant. Specialized in Business Establishment, Leadership training, Online Marketing, Small groups and teams leadership and management, Curriculum Development, Constitution development and much more.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.

8 + 11 =

PO Box 1999, city, country
SLP 1999, mji, nchi