TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

Tanzania Nakupenda kwa moyo wote” ni wimbo wa kizalendo kwa wazelendo wa kweli wa Tanzania. Imba wimbo huu kwa moyo wa kweli na rohoni utakuambukiza kuipenda na kujitoa kwa ajili a nchi yako pendwa ya Tanzania


 1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
  Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana

Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

 1. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
  Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,

Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

 1. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
  Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru

Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

 1. Tanzania Tanzania, Kaaribu wasio kwao,

Wenye shida na taabu, hukimbizwa na walowezi

Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee

Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa

 1. Tanzania Tanzania, watu wako ni wema sana
  Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena

Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli wee

Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi