Kuandika Andiko la Mradi

Kuandika Andiko la Mradi

Utangulizi

Uandishi wa andiko la mradi ni sanaa na ni utaalamu. Mwandishi wa andiko la mradi ni lazima awe na sanaa ya uandishi wa maandiko yenye kusomwa na watu na pia awe na elimu na uzoefu wa namna gani miradi ya kijamii inavyobuniwa, inavyopangiliwa, inavyotekelezwa, inavyosimamiwa, inavyotathminiwa na inavyohitimishwa.

Maelezo haya ni muundo tu wa sehemu kuu za Andiko la Mradi

Kasha la nje

Kasha la nje ni lazima iwe na kichwa cha habari, jina la taasisi , muda wa kuanza na kuisha kwa mradi na waandishi au mwandishi wa andiko hilo

Mfano

andiko la mradi - kasha la nje

Kasha la ndani

  1. Maelezo kwa ufupi au muhtasari wa mradi mzima: Utakuwa maeneo gani?, Walengwa ni akina nani elezea kwa jinsia?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
  2. Maelezo ya mradi: Elezea historia na wasifu wa taasisi itakayotekeleza na kusimamia huo mradi. Elezea pia eneo la mradi, watu, mila, shughuli za kiuchumi, imani na mambo yote ambazo zitaipamba andiko la mradi.
  3. Historia ya matatizo: Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo lilianza nkwa nani?
  4. Uchambuzi wa uhitaji: Kwanini tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki? Je, mradi ni suluhisho halisi na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
  5. Uchambuzi wa wadau wa mradi: Ni wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu, mchango wa wadau hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu?
  6. Mpango wa utekelezaji: Anza kwa kueleza Malengo ya mradi kuanzia lengo  kuu malengo ya muda mfupi na kati, shughuli za mradi ni zipi na unatekelezwaje katika jamii hii, viashiria vya ufanisi, viashiria vitapimwaje, vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali zilizopo na madhaifu/changamoto zinazohitaji kutatuliwa nk.
  7. Usimamizi wa mradi: Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?
  8. Masuala mtambuka: Chambua kama kuna uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala la mazingira linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na magonjwa yasiyotibika yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa mradi huu?
  9. Ufuatiliaji na tathmini ya mradi: Umepanga kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi huu? Uendelevu wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu kwa namna gani?
  10. Uendelevu wa mradi: Je kuna mipango madhubuti yatakayowezesha mradi kuendelea kuwepo hata baada ya ufadhili kuisha?
  11. Rasilimali Zitakazohitajika: Rasilimali ni pamoja na vitu, watu na pesa. Pesa zichambuliwe vizuri kupitia kwenye bajeti ya mradi: Ainisha ghrama za ununuzi wa vitu, malipo ya mishahara na gharama zingine zitakazohitajika ili kuendesha mradi

Kumbuka: Ninafundisha namna ya kuandika kwa urahisi andiko la mradi, pia ninaandika andiko la mradi kwa bei rahisi kwa vikundi, mashirika, vyuo, shule, makanisa, NGO, CBO na watu binafsi.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi