Kuna namna nyingi za kukaanga kuku ila leo ntakuonyesha jinsi ya kukaanga kuku kwa njia ya kisasa zaidi. Njia hii ni rahisi na inafanya  kuku ziwe na ladha nzuri na pia muonekano wa kuvutia zaidi.

Mahitaji kwa kuku mmoja:

  • Mayai 2
  • Unga wa ngano 1/2 kilo
  • Pilipilimanga kijiko 1(iliyosagwa)
  • Kitunguu swaumu vijiko  2 (iliyosagwa)
  • Tangawizi vijiko 2 (iliyosagwa)
  • Rangi ya chakula ½ kijiko
  • Limao 1
  • Chumvi ½ kijiko

Maandalizi kabla ya kuanza kupika:

  • Osha kuku vizuri kisha katakata katika vipande vidogo
  • Pasua mayai kisha yachanganye
  • Changanya unga, rangi ya chakula na mayai

Hatua za kufuata wakati wa kupika :

  • Katakata kuku katika vipande vidogovidogo kisha osha
  • Weka pilipilimanga, kitunguu swaumu, tangawizi,chumvi  na limao kwenye kuku kisha changanya
  • Chukua kuku mmoja mmoja kisha chomvya kwenye mchanganyiko wako wa mayai na unga
  • Hakikisha kuku wanapata mchanganyiko huo vizuri
  • Weka mafuta jikoni mpaka yachemke kisha tia kuku na uwaache waive mpaka wawe rangi ya brown
  • Unaweza kutia nakshi pia kuwekea kachumbari

Mfano ya kuku waliokaangwa :

 

ASANTE NA KARIBU