Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Kupitia Email kwa Kiswahili

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)

Utangulizi

Kuelekea maendeleo ya sayansi na teknolojia na hasa kwenye nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) makampuni na waajiri wengi sasa wanataka maombi ya kazi yafanywe kwa email au barua pepe.

Maombi ya kazi kupitia email husaidia yafuatayo:

  1. kuokoa gharama kama za uchapaji na usafirishaji
  2. kuokoa muda wa barua kutoka kwa muombaji mpaka imfikie mwajiri
  3. Kuharakisha pia mawasiliano baada ya maombi kutumwa

Kama utaomba kazi kupitia email zingatia yafuatayo:

  1. Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Daudi Joseph Masanja, email iwe hivi. daudijosephmasanja@gmail.com, NK. Angalau majina yako mawili yatokee kwenye email ID. Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama dumelamji@gmail.com au dijose@gmail.com mkereketwa@gmail.com NK
  2. Tumia pia email zenye kufuata weledi wa kimataifa. Mfano siwashauri watu kutumia email za microsoft, yahoo au zinginezo ambazo zinatumia very offensive security blocking policy. Mfano halisi ni huu email za Microsoft zinaongoza kwa kublock makundi mengi ya email duniani. Kwa hiyo ikitokea umetumiwa email na mwajiri ambaye email zake zimezuiwa na Server za microsoft ni wazi huo ujumbe wa kuitwa kwenye usaili hautakufikia na hivyo utakuwa umekosa hiyo kazi. Yahoo nao kwa mbali wanafuata. Gmail ndio mtoa wa huduma za email pekee yake ambaye hazuii email yeyote ila anatumia kitu kinachoitwa kwa kimombo “Intelligent Email Blocking Engine” email zako kama zinatia wasiwasi zinapelekwa kwenye spam folder. Kwa ushauri wangu email za Google yaani gmail ni wazuri na wanaongoza kwa kuwajali wateja wao kwa kutoa huduma nzuri na salama.
  3. Elezea vizuri kwenye kichwa cha habari yaani subject ya email unaomba nafasi ipi ya kazi. Waajiri wengine wanatoa kabisa kichwa cha somo kwa hiyo unatakiwa kukopi na kupaste. Usipofanya hivyo maombi yako yanaweza kuachwa na system kwani email kama hizi zinachujwa na mfumo wa kielectroniki kwa hiyo ukikosea kidogo tu imekula kwako wewe mwombaji.
  4. Kwenye email body au message eleza wewe ni nani? Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi? Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi) Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi. Pia eleze kwa ufupi: Kiwango chako cha elimu (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba) Uzoefu wako wa kazi (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba) Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani). Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wako tu (usiambatanishe vyeti au kitu kingine kwani hivyo utavipeleka wakati ukiitwa kwenye usaili) AU ambatanisha vitu hivyo kama mwajiri wako mtarajiwa anavitaka.
  5. Weka viambatanisho tu ambazo ulielekezwa utume, vile ambavyo hukuambiwa usitume maana vinaweza kukukosesha kazi. Waajiri wengi siku hizi wanapunguza mzigo wa maombi ya kazi ikiwa ni pamoja na package nzima ya maombi lakini pia na wingi wa waombaji. Ni rahisi sana kuchujwa kwenye chujio la mwanzo kama wewe umekiuka masharti ya wazi tu. Nasema ni rahisi kwa sababu waombaji ni wengi kwa hiyo waajiri wana aina fulani ya kuringa.
  6. Kwenye viambatanisho hakikisha vyote vina majina yanayoendana na kilichomo ndani. Mfano kama umeambatanisha Barua ya Maombi ya Kazi ya Mhasibu Msaidizi, weka jina la faili liwe na hayo maneno. Kama umeambatanisha CV kwenye filename ya CV weka CV ya …jiana lako NK. Mfano jina la barua ya maombi ya kazi iwe na jina la faili ya “Barua ya Maombi ya Kazi ya Mhasibu Msaidizi” na CV iwe na “CV ya Daudi Joseph Masanja”

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email

Yah:  Maombi ya Kazi ya ………………………………………………………………..(hii inawekwa kwenye email subject)
Simu: 075 xxxxxxx
Emal: daudijosephmasanja@gmail.com
12/8/2011

Ndg………………………………………….

Husika na kichwa cha somo tajwa hapo juu, mimi ni mhitimu wa sheria kutoka chuo cha ……………………… nimefanya kazi kwa miaka miwili na nina uzoefu kwenye sheria za makampuni na ajira. Napenda sana kujifunza mambo mapya na nina hamu ya kuleta mabadiliko kila mara. Tabia hii nimejijengea tangu utotoni kwani wazazi wangu walikuwa wakiniita mtoto mdadisi na mtukutu kwa sababu ya tabia hii ya kupenda kujaribu na kufanya jambo jipya kila mara.

Nimeambatanisha barua ya maombi ya kazi na wasifu wangu katika barua pepe hii

Kwa mawasiliano ya hara tafadhali piga namba hii (755XXXXXXX) wakati wote isipokuwa usiku wa saa nne mpaka 12.00 asubuhi. unaweza tuma maelezo kwenye barua pepe ya daudijosephmasanja@gmail.com

Nitafurahi nikiitwa kwenye usaili ili nidhihirishe kwako jinsi nitakavyowafaa kwenye kampuni yenu pendwa

Wako

Daudi Joseph Masanja

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi