Wadau wa mradi ni watu au taasisi ambazo zinahusika kwa naman moja au nyingine katika maendeleo ya eneo mradi ulipo. Wadau wanaweza kuwa ni wakazi, wafanyakazi, wageni, wafanyabiashara, au mashirika na taasisi mbalimbali kwenye eneo la mradi. Wadau wakitambuliwa na kutumiwa vizuri wanaweza kuongeza thamani kwenye matokeo ya mradi. Wasipotambuliwa na kutumiwa vizuri wanaweza aidha kuwa na madhara kwenye mradi au mradi usinufaike kwa uwepo wao.
Kuna aina kuu nne za wadau wa mradi kama ifuatavyo:
- Wadau wenye matakwa yanayoendana na uwepo wa mradi
- Wadau wenye matakwa yanayokinzana na uwepo wa mradi
- Wadau wenye umuhimu kwenye mradi na
- Wadau wasio na umuhimu kwenye mradi
Hatua muhimu za kufanya:
- Kuwatambua wadau wote waliopo katika eneo la mradi
- Kutafiti ili kujua matakwa yao na umuhimu wao katika mradi
- Weka mikakati ya kuwashirikisha katika uendeshaji wa mradi kulingana na matakwa na umuhimu wao
Jedwali la kupima umuhimu wa kila mdau na ngazi ya ushirikishwaji
Ngazi ya ushiriki
Aina ya ushirikiano |
Ushiriki hauhitajiki kwa wadau hawa | Ushiriki katika ngazi ya kutoa taarifa tu | Ushiriki katika ngazi ya kutoa Ushauri | Ushiriki katika ngazi ya kuwa mshiriki mwenza | Ushiriki katika ngazi ya kudhibiti uendeshaji wa mradi |
Utambuzi wa mradi | *** | *** | *** | *** | *** |
Kupanga mradi | *** | *** | *** | *** | *** |
Kusimamia mradi | *** | *** | *** | *** | *** |
Kufuatilia na Kutathimini mradi | *** | *** | *** | *** | *** |
*** Taja majina yao hapa
Kumbuka: Mdau anaweza kutokea mara nyingi kwenye vyumba kwenda chini lakini sio kwenda kulia
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |