Jinsi ya Kupata Ufadhili wa NGO au CBO

Hatua 4 Rahisi za Kupata Ufadhili wa CBO/NGO

1) Anza kwa kufanya mwenyewe kwanza
2) Hamasisha Watu Wako wa Karibu
3) Hamasisha ufadhili mdogo na mkubwa kwa watu wa mji wako
4) Toka nje ya mipaka ya mji/nchi yako

1) Anza kwa kufanya mwenyewe kwanza

Anza kutumia mali zako, nguvu yako, akili yako na muda wako kuyafanya baadhi ya yale yalio kwenye malengo ya NGO/CBO yako. Hii itahamasisha sana watu wengine wakuunge mkono kwani wataona kwamba hiyo huduma unaibeba kama wito zaidi ya ombaomba tu.

Mfano Robert Piece (Maarufu kama Bob Piece) ambaye alikuwa mwinjilisti wa kimataifa kutoka Marekani na mwanzilishi wa Shirika la World Vision International alipoenda kuhubiri injili kule China, alikutana na mtoto yatima, baba yake alifariki kwenye vita na mama yake alimtelekeza. Maono ya kunzisha shirika la kuwahudumia watoto kama hao ilianza moyoni mwake. Alikachukua kale katoto akampleka kwenye kituo cha kulelea watoto yatima na kuacha dola 5 na kuahidi kutoa dola kama hiyo kila mwezi ili isaidie kituo hicho kumlea yule mtoto. Aliahidi pia kwenda Marekani kuwahamasisha marafiki zake nao wachangie kituo kile.

2) Hamasisha Watu Wako wa Karibu

Wahamasishe majirani, ndugu, rafiki na jamaa wa karibu wakuunge mkono kwa kujitolea ( volunteering)

Mfano ule wa Bob Piece unaendelea…

Robert Piece aliporudi Marekani aliwahamasisha marafiki na jamaa zake wachangie kituo kile cha huko China na wakafanya hivyo kwa urahisi kwa sababu Robert alianza mwenyewe kujitolea.

Ndugu, jamaa na marafiki wataguswa na story yako kama wewe mwenyewe umeanza kwa kujitoa kwa kutumia mali zako, pesa zako, nguvu yako, akili yako na muda wako kwenye hiyo huduma.

3) Hamasisha Ufadhili kwa Watu wa Mji Wako

Hiyo ya kwanza na pili ikifanikiwa, anza sasa kuwahamasisha watu wa mji wako au nchi yako.

Usikimbilie Ulaya na Marekani wakati hata mashirika, taasisi na makampuni yaliyoko kwenye mji au nchi yako hujawafikia na hitaji la kusaidiwa kwenye miradi ya kijamii.

Makampuni mengi ya kibiashara hata zile changa huwa zinatenga kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kuchangia kazi za kijamii yaani corporate social responsibility. Zingine hata kama hazikutenga zikiendewa zitatoa mchango kwa ajili ya kusaidia jamii.  Pesa hizi huwa mara nyingi haziombwi na kwa hiyo hazitumiki kutoka mwaka hadi mwaka. Unashauriwa basi kuweka utaratibu mahsusi wa kuzifikia hizo taasisi zilizo karibu na wewe lakini hakiksiha kwamba namba 1 na 2 hapo juu umetimiza. Utakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuchangiwa iwapo wewe mwenyewe na marafiki zako wamefanya jambo la kimaendeleo kwa kuchangia hiyo miradi. Uwe na ushahidi wa kwamba miradi hiyo imechangiwa na wewe na marafiki zako ili ihamazishe wengine kutoa. Hapa namaanisha uweke kumbukumbu zako za mapato na matumizi vizuri na zikaguliwa na Auditor anayetambulika na Taasisi husika. Wachangiaji wengine wanaweza kukuuliza kuhusu hiyo ripoti ya ukaguzi kwa uhakiki zaidi.

4) Toka Nje ya Mipaka ya Mji au Nchi Yako Sasa

Sasa unaweza kutoka nje ya mipaka ya mji au nchi yako kwa ujasiri kwa ajili ya kuomba nguvu zaidi ya kuyafikia malengo ya NGO au CBO yako. Wageni wakiona kwa kiwango kikubwa wenyeji wanachangia miradi kwa ajili ya wenzao, na wao watashawishiwa kwa urahisi na kwa kutoogopa kukuunga mkono kwa kutoa michango yao ya mali, pesa au kujitolea taaluma yao NK. Hakikisha tu unaweka kumb ukumbu ya uchangiaji wote kuanzia ule wa kwako, jamaa zako wa karibu, wachangiaji wa mji au nchi yako ili upate nguvu ya kusaidiwa na watu au mashirika ya nje.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

__________________________________________________
We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi
https://www.googletagmanager.com/gtag/js?id=UA-27777942-1