UTANGULIZI

Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni na biashara kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili jina la biashara imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI

Hatua #1: Taarifa za msajili, mmiliki au wamiliki wa biashara

 1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
 2. Simu ya kiganjani
 3. Barua pepe yaani email

Hatua #2: Taarifa za biashara

 1. Aina ya biashara mtu binafsi, washirika au shirika
 2. Jina la biashara

Hatua #3: Ofisi ya biashara (Business Location)

 1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
 2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
 3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)
Mfano wa anuani ya makazi yasiyopimwa
 1. Region: Arusha
 2. District: Arusha CBD
 3. Ward: Unga Limited
 4. Postal: code 23107
 5. Mtaa: Viwandani,
 6. Kitongoji: Olevolosi
 7. Karibu na kiwanda cha ATOZ
Mfano wa anuani ya makazi yaliyopimwa
 1. Region: Arusha
 2. District: Arusha CBD
 3. Ward: Kati
 4. Postal code: 23102
 5. Street: New Livingstone Street
 6. Road: New Livingstone Road
 7. Plot number: 91
 8. Block number: F
 9. House number: 704

Hatua #4: Shughuli za Biashara (Business Activities)

 • Taja shughuli za biashara kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification

Hatua #5: Taarifa za Wamiliki (Business Owner’s Information) pamoja na Akaunti ya Benki kama ipo

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #6: Taarifa za Akaunti ya Benki Zingine kama ipo (Business Bank Account Information)

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #7: Taarifa za Wawakilishi (Person who can update ORS Information)

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)

Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-

 1. Consolidated form iliyosainiwa wamiliki wote wa biashara
 2. Viambatanisho vingine vinakuja

Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)

Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini

 1. Kusajili biashara = TZS. 15,000
 2. Kuhifadhi nyaraka na = TZS. 5,000/mwaka
 3. Stamp Duty = TZS. 500

Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)

Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni

 1. Kuweka Benki: Kwa njia ya kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
  Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha:  Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako

Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

Soma zaidi kuhusu jinsi ya kufanya malipo BRELA Kupitia Simu Yako

HITIMISHO NA USHAURI

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka karatasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:

 1. Nashauri kama unataka kusajiliwa jina la biashara au kampuni kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia  mawasiliano
 2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana namikupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano