Ukaguzi ni utaratibu wa kuyapitia mahesabu ya taasisi ili kuona kuwa pesa zimetumika sawasawa na makusudio yake. Ili kuona kama tamaduni na nidhamu ya matumizi ya fedha yalizingatiwa na kufuatwa.
Mahesabu yanayopitiwa ni
- Taarifa za fedha – Financial Statements,
- Akaunti za fedha – Management Accounts,
- Ripoti za fedha – Management Reports,
- Rekodi za fedha – Accounting Records,
- Ripoti za utendaji – Operational Reports,
- Ripoti ya mapato – Revenues Reports,
- Ripoti ya matumizi – Expenses Reports
- Nk – ETC
Kuna ukaguzi wa aina mbili
- Ukaguzi wa nje – External Audit
- Ukaguzi wa ndani – Internal Audit
Iwe ni ukaguzi wa nje au wa ndani inazaa kaguzi zifuatazo
- Ukaguzi wa kushtukiza – Forensic Audit
- Ukaguzi wa kupangwa – Statutory Audit
- Ukaguzi wa Mahesabu – Financial Audit
- Ukaguzi wa Kodi – Tax Audit
Wakaguzi wa fedha wataangalia yafuatayo
- Kuafanya mkutano na wafanyakazi unaoitwa Entry Meeting ili kuelezea mambo muhimu yanayotakiwa wakati wa zoezi la ukaguzi kama ushirikiano, uwazi, kueleza dhumini la ukaguzi, maksi zinatolewaje, na repoti zinatolewaje, Mswali na majibu ili kuweka mambo sawa
- Uwepo wa sera za fedha na mali za kampuni katika viwango vinavyotambulika
- Uwepo wa mpango kazi
- Uwepo wa sheria za udhibiti wa ndani
- Uwepo wa watumishi husika katika viwango vinavyotambulika
- Uwepo wa akaunti za benki na watia saini
- Uwepo wa register ya mali za kampuni
- Uwepo wa rekodi ya mapato na matumizi ya fedha
- Uwepo wa ripoti za fedha katika viwango vinavyotambulika
- Kuhoji watumishi juu ya utamaduni wa kutumia fedha
- Kuafanya mkutano na wafanyakazi unaoitwa Exit Meeting ili kutoa shukrani, kuelezea baadhi ya mambo ya awali yaliyojitokeza yanayohitaji uwajibikaji wa wote, kukumbushia kusudi la ukaguzi, na maksi yanavyotolewa, kuelezea kuhusu repoti zitatokaje, lini, maswali na majibu, ushauri wa awali kuhusu nini kifanyike ili kukabiliana na mambo ya msingi yaliyojitokeza
- Kuandika ripoti kwa manajimenti ya mambo yaliyoonekana hayafai na yanahitaji amelezo
- Kutoa ripoti kuu tatu za fedha ambazo ni Mapato na matumizi, cashflow, balance sheet
- Kutoa ripoti ya mwisho ambayo itasainiwa na wakurugenzi ikionyesha utendaji kazi katika updande wa fedha na mapendekezo ya mambo ya kurekebisha / kuzingatia ili taasisi ifanye vizuri zaidi na fedha na mali za kampuni ziwe salama
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |