Usajili wa vikundi au vicoba

Taratibu za Kufuata Katika Kusajili Kikundi, Vicoba

Vicoba ni nini?

Hivi ni kikundi au vikundi vya watu 20 hadi 30 hivi wanaofahamiana ambao wameamua kuunda kikundi ili kupata huduma za mafunzo mbalimbali, huduma za kifedha na kuwekeza miradi ya pamoja kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Wanachama wa vicoba vingi hukutana mara moja kila wiki na wengine wachache wasio na nafasi ya kukutana kila wiki hukutana mara moja kila mwezi au robo mwaka nk.
Ili kurasimisha au kusajili vikoba, taratibu zifuatazo zitasaidia kuanza na kuendelea na mchakato mpaka umalize usajili au urasimishaji.
Mambo yafuatayo ni lazima ziwepo
  1. Wanachama wasiopungua 20 wawepo
  2. Katiba ya Kikundi au kikoba au kicoba
  3. Dondoo za kikao cha wanachama kilicho keti kujadili na kuamua kusajili kikundi
  4. Barua ya kuitambulisha kikundi kwa ofisi ya mtendaji wa kata
  5. Barua ya maombi ya kurasimisha au kusajili kikundi itumwe kwa mkurugenzi wa halmashauri kikundi kilipo nakala (kk) ya barua ya maombi ziende kwa
  • Mwenyekiti wa mtaa – mpokeaji wa nakala ya barua
  • Afisa mtendaji wa kata – mpokeaji wa nakala ya barua
  • Afisa wa maendeleo wa kata – mpokeaji wa nakala ya barua

NB: Kwa maelezo zaidi juu ya usajili na mabadiliko yake mtembelea afisa wa maendeleo wa kata yako

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi