UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.
Hatua zifuatazo zinawawezesha wamiliki, wasimamizi wa makampuni na biashara kuingiza taarifa zao kwenye tovuti ya BRELA
Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za kampuni chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano
Hatua #1: Taarifa za msajili
Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).
Taarifa zenyewe ni:-
- Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
- Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
- Jina la kampuni
- Kazi zitakazokuwa zikifanywa na hiyo kampuni tarajiwa (Activity description)
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
- Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
- Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- TIN
- Simu ya kiganjani
- Barua pepe yaani email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
- Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- Simu
- Barua pepe – email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
- Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
- Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
- Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
- Simu
- Barua pepe – email
- Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
- Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
- Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
- Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
- Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
Hatua #8: Viambatanisho
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
- Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
- Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
- Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
- Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili
Malipo ya ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
- Kusajili kampuni
- Kuhifadhi nyaraka na
- Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni
- Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa
- Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo
HITIMISHO NA USHAURI
Nashauri yafuatayo:
- Nashauri kama unataka kuingiziwa taarifa za kampuni kwa haraka wasiliana nasi kwa mawasiliano
- Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
- Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
- Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Gharama za usajili wa kampuni BRELA kwa ufupi ni
- Gharama za usajili wa kampuni ndogo ya chini hisa za Shs milioni ni Shs. 1,117,200
- Gharama za usajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 1 hadi milioni 5 ni Shs. 1,297,200
- Gharama za usajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 5 hadi milioni 20 ni Shs.1,432,200
- Gharama za usajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 20 hadi milioni 50 ni Shs.1,512,200
- Gharama za usajili wa kampuni ya kati hisa za zaidi ya Shs milioni 50 ni Shs. 1,862,200
- Gharama za usajili wa kampuni isiyo na hisa ni Shs. 1,372,200
- Gharama za usajili wa jina la biashara ni Shs. 80,000
Hatua saba (7) muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara
- Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
- Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
- Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao – siku ya tatu
- Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
- BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
- Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho. Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
- Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF
Kumb:
- Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
- Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
- Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
- Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
- Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.
Maelezo zaidi ya namna ya kusajili biashara au kampuni BRELA
- Hatua 10 Rahisi za Kufuata ili Kusajili Kampuni Kupitia Website ya BRELA
- Hatua 10 Rahisi za Kufuata ili Kusajili Jina la Biashara Kupitia Website ya BRELA
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |