Tafsiri ya Maneno

Alama za biashara (Trademark, Trade-Mark, Trade Mark) ni jina au nembo iliyobuniwa na kutambulika kisheria kutambulisha bidhaa fulani miongoni mwa bidhaa shindani.

Alama za huduma (Servicemark, Service-Mark, Service Mark) ni jina au nembo iliyobuniwa na kutambulika kisheria kutambulisha huduma fulani miongoni mwa huduma shindani.

Alama ya biashara au huduma inaweza kuwakilishwa kwa jina tu, Nembo tu au zote mbili.

Gharama za kusajili

Gharama za kusajili alama za bishara au huduma BRELA (Gharama hizi ni pamoja na gharama za BRELA)

  1. Gharama kuu ni Shs. 150,000/=
  2. Gharama za kurudia baada ya masahihisho ni Shs. 50,000/=

Masharti ya usajili

  1. Mteja anawajibika kisheria na alama za biashara au huduma
  2. Mteja antakiwa kutoa taarifa zote pamoja na alama za biashara au huduma ndani ya siku 5
  3. Zikipita siku tano, gharama ya Shs. 50,000/= itahusika

Sababu za marekebisho

  1. Taarifa zilizotolewa zina kasoro
  2. Usajili umekataliwa na BRELA kwa sababu zilizo nje ya agent