Contract Mkataba

Mkataba wa Kupangisha Chumba, Nyumba ya Kuishi, Ofisi au Biashara

Mkataba wa Kupangisha Nyumba

 

Mkataba huu tumeuweka leo tarehe …………………………………… kati ya

………………………………………………………………………………………… wa simu na……………………………………

(Ambaye kwa maana ya mkataba huu ataitwa “Mpangishaji”)

Na:………………………………………………………………………………… wa simu na……………………………………

(Ambaye kwa maana ya mkataba huu ataitwa “Mpangaji”)

Mpangishaji na Mpangaji wanakubaliana yafuatayo:

1)            Kwamba muda wa Upangishaji ni miezi………… na utaanza tarehe ………………. na kuisha tarehe ……………………………………

2)            Kwamba upangaji huu ni kwa matumizi ya ………………..……………………………………

1)            Kwamba kodi ya upangishaji ya nyumba/chumba ni TZS. ……………………… kwa mwezi ambayo italipwa kwa mkupuo wa miezi ……………………………

2)            Kwamba kodi ya awali ya Shs. ……………………………… italipwa wakati wa kusaini mkataba huu na kodi za awamu zingine zitakuwa zikilipwa katika tarehe hizi ………………………………………………………………………………………………….

3)            Kwamba kama mpangaji hajalipa kodi baada ya siku …… atawajibika kulipa riba ya …………. kwa mwezi kwa kila deni linalodaiwa

4)            Kwamba mpangaji atawajibika na ukarabati kwa uharibifu utakaosababishwa na yeye au jamii yake.

5)            Kwamba endapo ukarabati utaadhiri sura na ramani ya awali ya nyumba/chumba basi mpangaji ni lazima apate kibali na maelekezo ya kimaandishi kutoka kwa Mpangishaji

6)            Kwamba mpangaji atagharamia ukarabati wowote utakaofanyika ambao haukuwa kwenye makubaliano ya awali ya upangaji.

7)            Kwamba mpangaji atawajibika na kulipia huduma muhimu kama za maji safi na taka, ada za takataka, ada za ulinzi na umeme nk.

8)            Kwamba mpangishaji anayo mamlaka ya kuweka mfumo mzuri wa kuchangia huduma za maji safi na taka na umeme au kusitisha huduma hizo

9)            Kwamba kama mpangaji katimiza masharti yote ya mkataba huu ikiwa ni pamoja na kulipa ada zote kwa wakati, mpangishaji au mwakilishi wake hatambugudhi mpangaji katika kipindi chote cha mkataba huu

10)        Kwamba mpangaji atakabidhi nyumba kwa mpangishaji wake kama alivyopewa wakati wa kukabidhiwa nyumba na mpangishaji

11)        Endapo Kutakuwepo na Mgogoro wowote, taratibu za Usuluhishi Itakuwa kama Ifuatavyo.

a)      Kwamba wahusika watakutana pamoja na kumaliza tofauti zao mezani

b)      Kwamba kama tofauti itakuwa bado haijaisha, kesi inatapelekwa kwa balozi wa nyumba kumi.

c)       Kwamba ikishindikana kwa balozi wa nyumba kumi mgogoro utapelekwa kwa mwenyekiti wa kitongoji/mtaa

d)      Kwamba ikishindikana kabisa kwenye kitongoji/mtaa, mhusika anayedhani hajatendewa haki anayo haki ya kupeleka mgogoro kwenye vyombo vya juu kwa usuluhishi zaidi.

12)  Kubadilishwa au kuboreshwa kwa mkataba

a)      Kwamba mpangishaji anayo haki ya kubadili au kuboresha mkataba huu muda wowote kadri hali itakapolazimu ili kukidhi haja ya mabadiliko ya muda, sheria/masharti na uhitaji wa mpangaji na/au Mpangishaji kwa makubaliano ya pamoja

b)      Kwamba endapo mabadiliko hayakumhusisha mpangaji, mkataba ukisha boreshwa utaanza kutumika kipindi cha mkataba unaofuata

13)              Kwamba notisi ya mabadiliko ya kodi yatatolewa na Mpangishaji si chini ya siku 30 kabla ya mkataba wa zamani kuisha

14)  Kusitisha Mkataba

a)      Kwamba notisi ya kusitisha mkataba kwa mpangaji au Mpangishaji utafanywa kimaandishi si chini ya siku 30 kabla ya siku ya kukatisha mkataba au kabla ya mkataba uliopo kuisha.

b)      Kwamba kama usitishwaji wa mkataba utafanywa na Mpangishaji kwa ridhaa yake mwenyewe, Mpangishaji atawajibika kurudisha pesa zote zilizobaki za mkataba pamoja na notisi ya kimaandishi ya siku 30 bure.

c)       Kwamba kama usitishwaji utafanywa na mpangaji kwa ridhaa yake mwenyewe, au kama usitishwaji utafanywa kwa sababu mpangaji kakiuka moja ya vipengele katika mkataba huu, kodi iliyolipwa haitarudishwa na kama mpangaji anadaiwa kitu chochote atawajibika kulipa kabla ya kuhama vinginevyo taratibu za kisheria za madai zitafuata mkondo wake.

15)  Sababu zitakazofanya mpangaji akatishiwe mkataba wake

a)      Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake kuwa mgomvi kwa wenzake hata baada ya kuonywa bila mafanikio

b)      Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake kuwa kero kwa wenzake hata baada ya kuonywa bila mafanikio

c)       Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake kutumia vyombo vyenye kuhatarisha usalama wake na jamii yake, majirani au mali za watu na mazingira – hii haitaji kuonywa.

d)      Ikigundulika kuwa mpangaji au mmojawapo wa jamii yake anafanya mojawapo ya shughuli zifuatazo: Ugoni, ushoga, usagaji, umalaya, madawa ya kulevya, wizi, utapeli, mihadharati, kutoa taarifa za kufanikisha uhalifu wowote na shughuli yeyote iliyopigwa marufuku

e)       Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake kufanya shughuli yeyote inayoadhiri wengine kiuchumi au kiafya

f)        Kwamba mpangaji anachelewesha kodi mara kwa mara bila ridhaa ya Mpangishaji (kodi itahesabika imecheleweshwa kama itakuwa ikilipwa zaidi ya siku …. ya tarehe halali ya kulipa)

g)      Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake kusababisha uchafu wa kwake mwenyewe, jamii yake au mazingira ya nyumba

h)      Kubadili matumizi ya nyumba kinyume na mkataba huu bila idhini ya kimaandishi ya Mpangishaji

i)        Kutumia bila kuchangia au kuchelewesha mara kwa mara uchangiaji wa huduma kama maji na umeme nk.

j)        Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake hashirikiani na wapangaji wenzake kwenye mambo ya msingi kama vile usafi, usalama nk)

k)       Mpangaji au mmojawapo wa jamii yake atavunja mojawapo ya vipengele katika mkataba huu

16)  Mkataba na Sheria za Nchi

a)      Kwamba mkataba huu haukukusudiwa kwa vyovyote vile kupingana na sheria yeyote ya nchi, ikitokea moja ya vipengele Katika mkataba huu vinapingana na sheria yeyote ya nchi basi sheria hiyo ya nchi itachukuliwa kama sehemu ya mkataba huu dhidi ya kipengele husika.

17)  Kuafiki Mkataba

a)      Kwamba mkataba huu tumeuweka tarehe tajwa hapo juu hapa mtaa wa ………………………… Kata ya ………………………. Katika mji wa ………………………………………

b)      Kwamba tukiwa na akili zetu timamu, bila kulazimishwa au kushawishiwa na mtu yeyote tumeweka sahihi zetu kama ishara ya kuusoma, kuuelewa na kukubaliana na masharti yote yaliyotajwa katika mkataba huu na kuahidi kutekeleza kwa moyo wote

c)       Kwamba tunakubali kukabiliwa na adhabu zitakazoambatana na kukiuka moja ya vipengele katika mkataba huu

Jina Sahihi Tarehe
Mpangaji __________________ __________________ ____________
Shahidi __________________ __________________ ____________
Mpangishaji __________________ __________________ ____________
Shahidi __________________ __________________ ____________
Balozi wa nyumba kumi __________________ __________________ ____________
M/Kiti wa Kitongoji/

Mtaa

__________________ __________________ ____________
 

Mhuri wa mwenyekiti.

 

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi