Katika maisha yangu nimejifunza yafuatayo
- Kama huelewi, sikiliza tu
- Kama huelewi, soma tu
Jifunze kusikiliza wengine hata kama huelewi au kusoma unachotakiwa kusoma hata kama huelewi.
Niliwahi kufaulu mtihani fulani bila kuelewa baadhi ya topics, ila nilitii hii kanuni ya pili ya kusoma tu. Nilichukua mtaala wangu nikaangalia natakiwa nisome wapi nikachukua vitabu vilivyopendekezwa kwenye mtaala nikasoma, sehemu kubwa nilkuwa ninasoma bila kuelewa. Cha kushangaza wakati wa mtihani, nilikutana na maswali niliyokuwa nasoma, nilikopi na kupaste kama wasemavyo waingereza. Wau mtihani sio tu nilifaulu bali nilikuwa wa kwanza darasani.
Katika filamu ya Colombian, kabla wazazi wake hawajauawa, binti wa kama miaka 10 ambaye ndie mhusika mkuu kwenye hiyo movie anapewa maagizo na baba yake (ambaye alijua atauawa na mke wake kwa sababu ya mahusiano mabaya na rafiki yake ambaye ni tajiri sana) ya namna ya kwenda kwa mjomba wake anayeishi Califonia. Mtot kwa mshangao na mshutuko mkubwa anamuambia baba yake sielewi kitu. Baba akamuambia hivi
“You don’t need to understand, you just have to listen!”
“Huitaji kuelewa, wewe sikiliza tu!”
Nakushauri na wewe mfuasi wa kivuyo.com kuwa katika maisha sio lazima kila kitu uelewe, kuna mambo utakazozielewa na Mungu abarikiwe ila kuna ambazo hutazielewa, lakini zote unatakiwa kusoma au kusikiliza ili ufaulu. Hivyo jenga tabia ya kumsikiliza mwenzako, mwalimu, Radio, kuangalia TV, au kusoma vitabu, majarida, tovuti nk hata kama kuna baadhi ya maeneo huelewi ali mradi unachokisikiliza kuangalia au kusoma ni muhimu katika maisha yako au taaluma yako.
- Kama huelewi, sikiliza
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |