Tathmini ya mradi au Project evaluation ni zoezi la kuchanganua miradi inayoendelea au zile zilizokwisha muda wake kwa lengo la kuchunguza kama rasilimali watu, vitu na pesa zilizotumika zimeleta tija na malengo yake yamefikiwa kwa kiwango gani.

  • Je matumizi ya rasilimali iliendana na mpango wa mradi?
  • Je mafanikio endelevu yatafikiwa au yamefikiwa?

Kuna tathmini za aina mbili

  1. Tathmini ya kati – Mid-term Evaluation
  2. Tathmini ya mwisho – End of project evaluation

Tathmini ya kati –hufanywa wakati mradi unaendelea na huwa mara nyingi kila baada ya mwaka inafanywa ili kujua kama malengo yanafikiwa na tunakwenda sawasawa na tulivyopanga. Pia kama kuna changamoto zishughulikiwe haraka ili tuenbde sawa na malengo yafikliwe kama ilivyopangwa

Tathmini ya mwisho – hufanywa baada ya mradi kufikia muda wake wa kufungwa. Mara nyingi tathmini hii hufanyika miaka 2 au 3 baada ya mradi kufungwa. Matokeo ya tathmini hii itawasaidia wadau wote wanaofanya miradi ya maendeleo kwenye eneo husika kuanzia kwa serikali, walengwa na taasisi zingine hata waliosimamia mradi kama wataanzisha mwingine watayatumia matokeo hayo kujifunza. Hata wakipanga kuanzisha miradi sehemu zingine watatumia matokeo ya tathmini hiyo kuboresha utendaji kazi

Mambo yanayotakiwa ili kutekeleza tathmini

  1. Watu- wenye ujuzi mbalimbali, wengine wa kuhiji, kugawa madodoso, kutayarisha madodoso, kuingiza kwenye kompyuta nk
  2. Vitendea kazi – gari, kalamu, madaftari, kompyuta, ofisi, nyaraka muhimu za mradi, nk.
  3. Mikutano ya watumishi, walengwa na viongozi wa taasisi na serikali
  4. Muda wa kutosha – kulingana na ukubwa wa mradi inaweza kuwa ni siku chache mpaka miezi kadhaa