Wasifu wa Lemburis Kivuyo – Mshauri/Consultant Wa Biashara

Mafunzo ya Ujasiriamali
Mafunzo ya Ujasiriamali

Wasifu wa Lemburis Kivuyo ni pamoja na kuwa mshauri wa biashara na TEHAMA katika kubuni biashara, na miradi, kuanzisha na kusimamia ili ilete faida iliyokusudiwa.

Ninafanya ushauri wa miradi ya jamii, biashara na kompyuta (TEHAMA) kupitia mafunzo ya ndani na kitaasisi, maeneo mahsusi yakiwa ni ushauri wa kuandika na kufundisha mpango wa biashara, mpango kimkakati, Andiko la Biashara / Mradi, usimamizi wa mfumo habari. Ushauri wa mtandao na mawasiliano, masoko masafa,  uongozi na mengi zaidi.

Tovuti pia inatoa mafunzo na taarifa za bure. Vitu vyovyote vya bure vinavyotolewa hapa ni mali ya wamiliki husika na hati miliki ni ya kwao. Ni wajibu wako kufungua na kusoma maelezo husika ya hati miliki kama vile leseni, mkataba, masharti ya matumizi kabla ya kutumia hati au programu.

Lemburis Kivuyo ni mwenye hamu kuu ya kujifunza kutoka kwa wengine, mu wazi, tayari kuwaelimisha wengine. Kwa kutumia utumishi wake kwa muda mrefu na miradi jamii, biashara na teknolojia ya kompyuta. Marafiki wake wengine wa karibu humwita “mchawi wa komyuta”.  Lemburis amekuwa mratibu wa miradi kwa zaidi ya miaka 10.

Yeye ni muasisi wa InfoCom Center Limited (kampuni binafsi ya kufundisha, kushauri na kufanya shughuli za biashara, kompyuta na miradi ya jamii) jijini Arusha.  Muasisi mwenza wa taasisi inatarajiwa kuwa chuo cha sayansi ya madini na ardhi cha Shinyanga (ESIS) na hivi karibuni mjumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa taasisi ya EWURACC

Ushauri wa kompyuta na TEHAMA

Kubuni ofisi dijitali

Kubuni na kuendeleza mfumo wa kompyuta katika maofisi kulingana na mahitaji ya ofisi, usalama wa taarifa, mafunzo ya ufahamu wa kompyuta (hasa usalama wake), sera ya usalama wa taarifa ndani ya kompyuta. Mafunzo ya Kompyuta kwa mameneja wasio na ufahamu wa TEHAMA.

Ushauri wa Mitandao na Masoko Masafa

Ushauri maalumu wa kitaalamu katika kubuni tovuti na blogu, kuhodhi tovuti, kuboresha upatikanaji wa mitandao katika search engines kama Google, Yahoo na Bing, Mshauri mahsusi wa dhana ya masoko masafa (yaani masoko kupitia mfumo wa elektroniki) (Electronic marketing AU-E Marketing), usalama wa mitandao, ukaguzi wa mitandao, usimamizi wa mitandao, ufuatiliaji wa utendaji kazi wa mitandao.

Ushauri wa Biashara

Uanzishwaji na Usajili wa makampuni, maandiko ya miradi na biashara, kuanzisha na kuendeleza biashara ndogondogo, utawala na uongozi wa biashara na jamii, wazo la biashara na mradi, Mchanganuo wa biashara na masoko, sera mbalimbali kama ya mali, fedha, wafanyakazi nk. Utafiti wa masoko masafa na ushauri masafa.

Ushauri wa miradi ya jamii na mashirika ya kijamii (CBO na NGO)

Uanzishwaji na usajili wa NGO na CBO,  Mzunguko wa usimamizi wa miradi (Project Cycle Management) Uwezeshaji, Utafiti wa awali (Baseline survey) Ubunifu wa mradi, Logframe Uchambuzi wa wadau, utafutaji wa raslimali, maandiko ya miradi, mpango mkakati, Katiba ya shirika, jumuiya, vyama na vikundi mbalimbali, Sera mbalimbali, utunzaji wa taarifa na uandikaji wa ripoti mbalimbali, uongozi na utawal bora, kuundan na kuwezesha kamati za miradi, tathmini ya miradi nk.  Maeneo mengine ni uwenzeshaji wa usimamizi wa majanga, na utatuzi wa migogoro.

Ushzauri na Kutengeneza Mitaala ya Elimu

Ninatoa ushauri maalumu katika eneo la kutengeneza mitaala unaofuata masharti na viwango vya Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania – NACTE. Hii inajumuisha na Utafiti na kuandika ripoti ya Mchanganuo wa Hali Halisi yaani Situational Analysis, Kuaanda na kusimamia pamoja na kuandika ripoti ya warsha ya ushauri wa kitaalamu yaani Consultative Workshop na Uandishi wa Mitaala yenyewe kuanzia ngazi ya Cheti (NTA Level 4 na zile za 5 na 6)

Mawasiliano:

Kivuyo Lemburis
Anwani ya Posta: 13143, Arusha-Tanzania, Afrika Mashariki

Simu / Simu: +255787665050 / +255755646470

Barua pepe: lembu [at] kivuyo [dot] com

Tovuti: www.kivuyo.com

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi