Tambi ya nyama

Jinsi ya Kupika Tambi ya Nyama ya Kusaga

Tambi ni chakula kinachotengenezwa kutoka kwa kinyunga cha unga na maji kuwa kama milia membamba inayopikwa katika maji au supu. Ni chakula muhimu katika nchi nyingi hasa Italia, China, Japani na Korea. Siku hizi zimeenea kote duniani na hapa Afrika Mashariki ni mojawapo ya chakula maarufu kwa watu wa rika zote. Aina zinazoliwa sana kimataifa ni pasta zenye asili ya Italia hasa spaghetti.

Kuna aina kuu nne za tambi:

  1. Tambi za mayai hutengezenzwa kwa kutumia kinyunga cha unga ya ngano na mayai
  2. Tambi za ngano hutengezewa kwa kinyunga cha unga na maji pekee pamoja na chumvi
  3. Tambi za mchele hutengenezwa kwa unga ya mchele pamoja na maji
  4. tambi kioo hutengenezwa kwa kutumia wanga ya maharagwe au viazi; hazina rangi zinaonekana kama kioo

Kuna njia mbalimbali za upishi kwa mfano

  • Tambi na mchuzi: tambi zinapikwa na kupelekwa mezani katika bakuli. Mchuzi wa majani, nyama au samaki huandaliwa kando na kumwagiliwa juu ya tambi kwenye sahani.
  • Tambi katika supu: tambi zinapikwa katika supu pamoja na mboga majani, nyama na viungo vingine. Kama viungo huhitaji muda mrefu mpaka kuiva tambi zinaongezwa katika supu kwa dakika za mwisho

Chakula hiki nikwaajili ya familia ndogo ya watu watano

HATUA YA KWANZA ANDAA VITU VIFU ATAVYO

  1. Tambi pact moja
  2. Nyama iliyo sagwa nusu kilo
  3. Mafuta yakupikia robo lita
  4. Chumvi pakiti moja
  5. Kitunguu maji kimoja
  6. Karoti moja
  7. Hoho moja
  8. Food color kijiko kimoja

HATUA YA PILI

  1. Andaa vitunguu kwa kukatakata
  2. chukua karoti menya na kukwanga
  3. chukua hoho katakata vizuri

HATUA YA TATU

  1. Bandika sufuria yako jikoni
  2. Weka mafuta acha yapate moto vizuri
  3. Weka vitunguu vikaange hadi viwe na rangi ya kahawia
  4. Weka karoti  geuza geuza
  5. Weka hoho geuza geuza
  6. Weka nyama iliyo kwisha sagwa
  7. Ikaange nyama uliyoweka vizuri ikiisha iva epu weka pembeni na ufunike

HATUA YA TATU

  1. Bandika maji rombo kikombe acha ya chemke
  2. Fungua pact ya tambi zitoe vunja katikati
  3. Maji yakiisha chemka  weka tambi jikoni
  4. Weka chumvi kijiko cha chakula
  5. Funika subiri kwa dakika mbili

HATUA YA NNE

  1. Funua chakula iliyofunikwa kwa dakika mbili
  2. Chukua mchanganyiko wa nyama
  3. Weka food color
  4. Geuza hadi zichanganyike
  5. Funika acha iive kwa dakika1
  6. Funua na kuepua
  7. Chakula kitakua tayari kwa kuliwa

Mifano ya vyakula vya tambi

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi