NGUZO 7 ZA MAFANIKIO BINAFSI

Nguzo 7 za Mafanikio Katika Elimu, Biashara

Utangulizi

Mafanikio ni hali ambayo kila mtu anapenda kuwa nayo na kuyafikia kila mara. Mafanikio humfanya mtu afarijike, ajisikie yuko salama, afurahi na kusonge mbele kwa ujasiri zaidi. Mafanikio humfanya mhusika kuwapenda wengine na kuwa mkarimu.

Ukikosa mafanikio unaweza kuwa na hasira, kukata tamaa, kutawaliwa na mfadhaiko wa akili, ulevi wa kupindukia, usinzi na kwa ujumla kuwa na tabia mbaya. Mtu anayeshindwa kufanikiwa huwa hana ujasiri na kila mara ametawaliwa na kushindwa, Ushirika mdogo na wenzake na sio mshauri mzuri kwa wengine

Tafsiri ya Mafanikio

Mafanikio ni ile hali ya kuweza kuyafikia kusudi au lengo lako la maisha ambalo Mwenyezi Mungu alikuumbia nalo. Kila mtu ameumbwa kwa kusudi na hilo kusudi ni wewe peke yako unalo jukumu la kulifikia. Mwingine aliumbwa kuwa mchungaji na mwingine kuwa mwalimu, kuna wengine wafanyabiashara na wengine wanasiasa nk. Ukiweza kufikia hilo kusudi au lengo ndipo tunasema mtu fulani kafanikiwa.
 
Haitoshi tu kusema kuwa mtu ana majumba, mashamba, magari au pesa nyingi benki ndio kafanikiwa. Inategemea ni kwa jinsi gani hizo pesa, majumba, mashamba, magari yana uhusiano kwanza na lengo kuu na pia umepataje hizo mali. Wengine wanapata kwa kuua, kula rushwa, kuiba, kutapeli. Mafanikio ya namna hii sio mafanikio ya kweli.

Nguzo 7

Ili ufanikiwe unatakiwa angalau kuzingatia nguzo 7 hapa chini:

  1. Kupanga
  2. Kupenda
  3. Kujiamini
  4. Kuvumilia
  5. Kuwa na mbadala
  6. Kuwajibika
  7. Kuweka vipaumbele

1) Kupanga

Wahenga walisema usipopanga umepanga kushindwa

Walisema pia usipokuwa na malengo kila lengo litakufikisha uendako

Mipango ndio inaweka majukumu ya kufanya. Mfano kama hujapanga la kufanya asubuhi waweza kulala hata mpaka jioni bila kuona kama kuna shinda yeyote.

Kupanga inaanzia kwa kuweka maono ya maisha yako. Unataka baada ya miaka 15/20 kuwa na mafanikio ya namna gani katika maeneo yafuatayo

  1. Kiuchumi
  2. Kiroho
  3. Kielimu
  4. Kisiasa
  5. Kijamii

i) Kiuchumi

Panga unatazamia kuwa na kampuni, ranchi, au ajira kwa ngazi ya mkurugenzi wa shirika, kampuni, taasisi ya serikali wenye mshahara mkubwa kulingana na wakati huo nk

ii) Kiroho

Upange kuwa maisha yako ya kiroho yatakuwaje baada ya muda huo, utakuwa mchungaji, mwinjiisti shekhe. Au hata kiroho utakuwa umepoa au umemuishia Mungu kwa undani zaidi nk

iii) Kielimu

Panga kama unategemea kuwa na digrii mbili au tatu baada ya miaka 15?

iv) Kisiasa

Kama unapendelea mambo ya siasa na upange kwamba baada ya miaka 15 utakuwa mbunge, rais wa nchi nk.

v) Kijamii

Utakuwa na familia ya namna gani, mke, watoto, elimu yao nk

2) Kupenda

Upendo tunaouzungumzia hapa ni passion. Huu ni upendo wenye kujitoa na kuwajibika zaidi. Kile kitu unachokifanya jitahidi sana ukipende. Kama ni kozi ya udaktari hakikisha unakipenda na udaktari wenyewe unaupenda kiukweli. Kwa maana hii hakikisha unachagua vizuri njia unayopita.Penda pia na hali ya mafanikio unayotarajia, mfano penda kuwa bilionea au msomi kwa ngazi ya udaktari, kama ni mwanafunzi penda ile hali ya kupata alama ya “A” kwa masomo yako nk

Usijipeleke kwenye unesi wakati kazi za kuwahudumia wagonjwa inakupa kinaa. Ukipenda kitu utakuwa tayari kuvumilia, kupambana na kukabiliana na changamoto zinazoambatana na eneo husika

3) Kujiamini (Kuwa mjasiri na kujiamini)

Ujasiri unakupa mambo mengi. Kujiamini, kuchukua hatua, kuamua na kutenda hata kama wengi wanakupinga na kukubeza

4) Kuvumilia

Kazi nyingi zina changamoto tena kubwa na nyingi. hakuna kazi rahisi duniani. Usipokuwa king’ang’anizi na mvumilivu utakuwa unatangatanga mara leo mikaa mara kesho umachinga wa bango mara kesho kutwa mfanyakazi wa nyumbani mpaka uzee unakukuta hujafanya kitu. Uvumilivu unakusaidia wewe kuijua kazi yako na changamoto zake na hivyo kukufanya wewe kuwa mtaalamu na guru wa eneo au sekta husika. Hata kama imechukuwa muda mrefu huko mbeleni utatumia gharama na njia rahisi kufikia malengo kwa sababu ya uzoefu ulionao kwenye eneo husika ambao umesababishwa na kuvumilia.

Kumbuka pia kuwa uvumilivu unaendana daima na kujifunza kutokana na changamoto unazokutana nazo njiani pamoja na kuweka mipango mbadala

5) Mpango mbadala (Kuwa na mpango mbadala)

Wahenga walisema kuwa

“Kushindwa ni dalili kuwa mpango wako wa kwanza haufanyi kazi hivyo weka mpango mwingine au mbadala”

Pia wahenga wengine walienda mbali zaidi na kusema

“Kushindwa ni fursa nzuri ya kufanya vizuri zaidi, safari hii kwa umakini zaidi”

Aliyegundua na kutengeneza taa alishindwa mara 10,000 na baadaye sana ndipo akagundua taa ambayo leo inatumulikia dunia nzima kuanzia majumbani, viwanja vya ndege na mpira pamoja na kwenye anga za juu

Wahenga walisema kuwa

“Kufanikiwa kupo kwa sababu kuna kushindwa na kushindwa kupo kwa sababu kuna kufanikiwa”

6) Kuwajibika (Kuwajibika na mafanikio au kushindwa kwako)

Daima watu wenye kufanikiwa wanawajibika kwa yale maeneo ambayo wanashindwa. Ukishindwa jisemee ni kwa sababu sikufanya vizuri kwenye eneo X na Y nk. Usianze kuwasingizia wenzako nk

Mfano wa timu ya mpira

Kama wewe ni mfungaji na ukashindwa kufunga bao la wazi, usiseme kuwa kiungo alikupa pasi mbovu au alipaiza juu sana

Sema kuwa nilichelewa kuuwahi mpira ndio maana nikashindwa kufunga. Siku nyingine nitajitahidi kuwahi mpira kama huo”

7) Kufanya kwa vipaumbele

Utekelezaji ndio hitimisho la mafanikio. Kama utapanga hata mipango 1,000 kama wewe hunatabia ya kutekeleza basi mafanikio sahau kabisa.

Kuna mitego mingi kwenye kutekeleza mambo uliyoyapanga

Kuweka Vipaumbele Kama Nguzo ya Kufanikiwa

Save

Save

Save

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi