Sehemu Muhimu ya Mpango wa Biashara

Sehemu Muhimu ya Mpango wa Biashara

Ukurasa huu utaelezea sehemu muhimu za mpango wa biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biashara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia watoa mikopo kama benki na taasisi za fedha, wawekezaji na viongozi wa kampuni/shirika

I.  Kasha la nje: Sehemu ya kichwa cha mchanganuo wa biashara.

  • Anuani ya kampuni
  • Anuani ya maofisa
  • Tarehe ya kuandika mchanganuo.
  • Anuani ya mtayarishaji/watayarishaji
  • Namba ya toleo la mchanganuo

II.  WAZO LA BIASHARA (AU MUHSTASARI)

Hii ni sehemu muhimu ya kueleza kusudio au wazo la biashara yako kwa muhstasari. Mambo mhimu hapa ni:

  • Kampuni/biashara itakuwa na ofisi zake wapi?, lini itaanza?, wasifu wa nani kaandika, unauza au kuzalisha nini?, soko lako ni lipi?, utawafikiaje wateja?, na makisio ya bajeti, mauzo, gharama na faida  (ambatanisha na chati na au jedwali
  • Nani ataongoza na uwezo wao
  • Malengo ni yepi na ni kwa nini unafikiri biashara itafanikiwa
  • Kama utahitaji mtaji kutokwa benki, wawekezaji au wenye hisa ni kwanini, kiasi gani?, utalipaje? na faida kwa wenye hisa, wawekezaji au benki

Kumb: Usiandike wazo la biashara kabla hujamaliza kuandika mchanganuo wako kwani ni muhstasari wa mchanganuo wenyewe

III.  YALIYOMO (Orodhesha sehemu muhimu tu katika mchanganuo wako)
IV.  SEHEMU YA I: MPANGILIO WA BIASHARA

Kuna nini hapa?

Sehemu hii iwe na muhstasari wa biashara na utawala au wahusika katika kusimamia biashara,yaani mameneja na watumishi wengine

A.  MUHSTASARI WA BIASHARA

Kwa ufupi eleza ni asili au mrengo au sekta gani biashara yako inaangukia, lini na kwa nini ilianzishwa. Pia eleza yafuatayo:

  • Maono
  • Wito
  • Eleza filosofia ya biashara yako na kwanini unafikiri ni tofauti na zingine. Yaani biashara yako itakuwaje ya kipekee
  • Mkakati (eleza mikakati uliyonayo kufanikisha biashara yako)
  • Mikakati yako inahusianaje?
  • Uchambuzi wa mazingira ya biashara (eleza nguvu na fursa ambazo zitawezesha biashara ifanikiwe. Pia eleza madhaifu na hatari zitakazokwamisha biashara) ni vizuri pia ueleze utazimuduje au kuzikwepa ili biashara isife

B.  MAELEZA JUU YA BIDHAA AU HUDUMA

  • Kama wewe unazalisha au ni muuzaji wa jumla, fafanua juu ya bidhaa zako, eleza kwa ufupi juu ya hatua za kuzalisha, jumuisha taarifa ya kampuni zinazokupa huduma pamoja na upatikanaji wa bidhaa na malighafi pamoja na mambo ya stoo.
  • Kama biashara yako ni ya uchuuzi: fafanua juu ya bidhaa zako, taarifa ya kampuni zinazokupa huduma pamoja na upatikanaji wa bidhaa pamoja na stoo.
  • Kama biashara yako ni ya kutoa huduma: orodhesha huduma za biashara

C.  HATIMILIKI

  • Elezea juu ya hatimiliki ya kazi zako, nembo za biashara na uhalali wa kumiliki kazi za wengine (Copyrights, Trademarks, and patent)
  • Ushahidi wa kusajili, picha na nk (Back up in Supporting Documents with registrations, photos, diagrams, etc )

E.  MFUMO WA KISHERIA BIASHARA YAKO

  • Elezea mfumo wa biashara yako na kwa nini umechagua iwe hivyo
  • Orodhesha wamiliki wa kampuni husika

F.  UONGOZI

  • Orodhesha watu watakaoendesha biashara yako
  • Fafanua kazi zao
  • Toa makadirio ya mishahara
  • Ambatanisha wasifu na taarifa zingine muhimu

G.  WAFANYAKAZI

  • Utakuwa na wafanyakazi wangapi katikk kila idara?
  • Je ni sifa zipi zinatakiwa?
  • Elezea juu ya mishahara
  • Elezea mahitaji ya baadaye ya wafanyakazi

H.  MASUALA YA FEDHA

  • Nani atahusika wapi kama vile mfumo utakaotumika, tehcnolojia, na idara nyeti za uhasibu

I.  MASUALA YA SHERIA

  • Nani atakuwa mwanasheria wa kampuni au masuala ya sheria yatafanywaje?

I.  MASUALA YA BIMA

  • Bima zipi zitawekewa bima na kampuni na kwa nini?

J.  USALAMA

  • Elezea jinsi gani vifaa vua stoo, ofisi na pesa zitalindwa

SEHEMU YA II: MPANGO WA MASOKO

Elezea juu ya mpango wa masoko na mgawanyiko wake na jinsi biashara yako itakavyoweza kushindana na kumudu ushindani wa kibiashara

Elezea yafuatayo

  1. Uchambuzi wa masoko
    1. Walengwa
    2. Washindani wako (Elezea juu ya uwezo wao na udhaifu wao)
    1. Mwelekeo wa soko
    2. Utafiti wa masoko ( njia, uchanganuzi wa takwimu, na utoaji wa matokeo)

C.  MKAKATI WA MASOKO

  • Bajeti itakuwaje ya masoko
  • Mbinu za kuuza na kuwafikia wateja
  • Usindikaji
  • Mfumo na Sera ya bei ya ushindani
  • Utambulisho wa biashara yako
  • Utunzaji takwimu za masoko
  • Mkakati wa kuuza kama vile kwa kutumia barua pepe, maajenti, nk
  • Mkakati wa kutoa motisha na promosheni katika mauzo
  • Mkakati wa kutangaza kama kupitia website, magazeti, TV, au NENO la MDOMONI
  • Mkakati wa mahusiano na wateja kama vile kushiriki kwenye tamasha mabalimbali nk
  • Kujisajili katika mitandao mbalimbali nk

D.  HUDUMA KWA WATEJA

  • Kazi gani utafanya kuimarisha huduma kwa wateja?
  • Elezea malengo ya kufikia ubora wa kutoa huduma

E.  UTEKELEZAJI WA MASOKO

  • Utendaji wa ndani
  • Kuwatumia wataalamu wa nje

VI. SEHEMU YA III: TAARIFA YA FEDHA

Elezea maeneo muhimu ya fedha itakayohusika katika sehemu hii

A.  Muhtasari wa mahitaji ya fedha

  1. Elezea kwanini unahitaji pesa?
  2. Unahitaji kiasi gani?

B.  MAELEZO YA MIKOPO

Ni lazima

(1) Ueleze ni jinsi gani utautumia huo mkopo ukipewa
(2) Ambatanisha na taarifa muhimu kama risiti, mikataba nk

C.  MAKISIO YA MZUNGUKO WA FEDHA (CASH FLOW FORECAST)

Hii ni ripoti muhimu ambayo huonyesha kama biashara yako itakuwa na uhai au la katika kipindi cha miaka 3 mpaka 5 ijayo

D. MAKISIO YA MAPATO KWA MIAKA 3 HADI 5

Kisia juu ya mapato na matumizi na faida ghafi itakayopatikana kwa miaka 3 hadi 5

E.  TAARIFA MAKISIO YA DHAMANI YA BIASHARA YAKO (PROJECTED BALANCE SHEET     )

Kisia mali, madeni na dhamani halisi ya kampuni yako ktk kipindi cha miaka 3 hadi 5

F.  UCHANGANUSI WA KUFIKIA MAUZO

Elezea ni kiasi gani cha mauzo kwa mwezi itawezesha kampuni yako kurudisha gharama

 

G.  TAARIFA YA FAIDA NA HASARA (PROFIT & LOSS STATEMENT)

Kisia juu ya mapato na matumizi na faida na hasara itakayopatikana kwa miaka 3 hadi 5

H.  MAHSABU YA UWIANO WA SEHEMU MUHIMU ZA BIASHARA (BUSINESS RATIOS)

Elezea uwiano kati ya bidhaa za stoo na mauzo, kati ya gharama za kununua bidhaa na mauzo, kati ya mishahara na mauzo nk

VII.  VIAMBATANISHO

A.  WASIFU WA WAFANYAKAZI

B.  RIPOTI YA FEDHA ZA WENYE HISA

C.  MIKATABA

E.  BARUA ZA MASHAHIDI

G.  BARUA ZINGINEZO ZA KISHERIA NK

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi