Namna ya Kuandika Wasifu wa Kampuni

Wasifu wa Kampuni ni muhstasari wa maelezo ya msingi unaoitambulisha kampuni kwa uma. Wewe fikiria ingekuwa wewe unaitafuta kampuni ikufanyie kazi yako ungependa kupata taarifa zipi?

Nafikiri ungependa kujua yafuatayo

Mawasiliano: Katika mawasiliano ungependa kujua yafuatayo: jina la kisheria la kampuni, jina la kiongozi mkuu, wadhifa wake, email yake, namba ya simu yake, tuvuti ya kampuni, anwani ya posta, sehemu ofisi ilipo, nchi ofisi ilipo na ukanda wa bara kama kampuni ni ya nje,

Muundo wa Kisheria na Umiliki: Ungependa pia kujua kama ni kampuni au shirika nk (kwa sababu ya faragha kupata kibali cha maandishi kutoka kwa wamiliki wa kampuni au unaweza orodhesha kulingana na uzoefu wao, elimu na jinsia nk unaweza baadaye kuwasilisha katika binafsi kwa walengwa orodhesha ya majina)

Namba ya Usajili: Kama kampuni imesajiliwa ungependa kujua namba ya usajili ili kujiridhisha kuwa ni kampuni halali. Kumbuka hii sio leseni

Jina la usajili: Ungependa pia kujua jina la kisheria lililotumika kuisajili hiyo kampuni

Tarehe ya usajili: Kuelezewa tarehe ya usajili

Muhstasari wa Kampuni: Ungependa kujau kwa ufupi kampuni inajishughulisha na kitu gani na kwa muda gani nk

Rasilimali za kufanyia kazi: Ungependa pia kuelezwa kama kampuni ian zana gani ili iweze kutimiza wajibu wake. Mafano mitambo, magari nk.

Wasifu wa Rasilimali watu: Ungependa pia kujua kampuni imejizatiti vipi na rasilimali watu ili kuweza kufikia viwango bora za utoaji huduma. Rasilimali watu ni pamoja na viongozi na wataalamu mbalimbali. Bodi ya wakurugenzi, washauri, maafisa na wataalamu wa muda

Kazi za msingi: Taja kazi za msingi ambazo kampuni inafanya kila siku au mara kwa mara

Kazi zinginezo: Taja pia kazi ambazo japo kampuni haizifanyi mara kwa mara lakini ianweza kufanya ikipewa

Masoko mahsusi: Taja ni amsoko gani kampuni imeyalenga

Uzoefu na Ufanisi: Hapa taja kazi zote mlizozifanya kwa ufanisi mkubwa

Uanachama na Urafiki: Taja taasisi ambazo kampuni yako ni mwanachama au wanamuungano fulani wa kikazi/kitaaluma nk

Marefarii: Taja watu au taasisi ambao sio wateja na wanaweza kukisemea vizuri kampuni ambao hawana uhusiano na kampuni kwa maana ya wakurugenzi au wafanyakazi na familia zao

Taja pia watu au taasisi ambao ni sehemu ya wateja wa kampuni yako ambao wanafurahishwa na huduma za kampuni

Mawasiliano:

Jina la Kisheria la Kampuni:Good-hope General Supply

Jina la Kiongozi Mkuu: Goodlove Herman

Wadhifa wake: Mkurugenzi

Email: gherman990@live.com

Simu: +255712356455

Tuvuti: www.jinalatovuti.co.tz

Anwani ya Posta: SLP 10000, Arusha, Tanzania

Sehemu ofisi ilipo: Arusha

Nchi ofisi ilipo: Tanzania

Ukanda wa bara: Afrika Mashariki

Muundo wa Kisheria na Umiliki

weka hapa kama ni kampuni au shirika nk  (kwa sababu ya faragha kupata kibali cha maandishi kutoka kwa wamiliki wa kampuni au unaweza orodhesha kulingana na uzoefu wao, elimu na jinsia nk unaweza baadaye kuwasilisha katika binafsi kwa walengwa orodhesha ya majina)

Usajili

Namba ya Usajili:

weka hapa

Jina la Usajili:

weka jina rasmi la usajili au jina linalotumika hapa

Tarehe ya usajili

weka hapa

Muhstasari wa Kampuni :

weka hapa

Rasilimali za kampuni

Rasilimali vitu

  1. Ardhi
  2. gari
  3. ofisi
  4. mashine na mitambo
  5. dhamani za ofisi
  6. nk

Rasilimali watu

orodhesha hapa

  • Bodi ya wakurugenzi = 7
  • washauri wa kudumu= 3
  • washauri wa muda = 4
  • maafisa wa kudumu= 5

Kazi za Msingi

Orodhesha yao hapa

Kazi Zinginezo

Orodhesha yao hapa

Masoko Mahsusi

Orodhesha yao hapa

Uzoefu na Ufanisi

Orodhesha kazi umefanya mafanikio hapa

Uanachama na Urafiki:

Taja taasisi ambazo kampuni yako ni mwanachama au wanamuungano fulani wa kikazi/kitaaluma nk

Marefarii

Watu au taasisi wanaotujua

Taja watu au taasisi ambao sio wateja na wanaweza kukisemea vizuri kampuni ambao hawana uhusiano na kampuni kwa maana ya wakurugenzi au wafanyakazi na familia zao

Watu au taasisi wateja

Taja pia watu au taasisi ambao ni sehemu ya wateja wa kampuni yako ambao wanafurahishwa na huduma za kampuni

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

__________________________________________________
We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi
https://www.googletagmanager.com/gtag/js?id=UA-27777942-1