Nini Maana Halisi ya Uzalendo na nani ni Mzalendo wa Kweli?

UTANGULIZI

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma.  Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa.

SIFA 10 ZA KUWA MZALENDO WA KWELI

Ili mtu aitwe mzalendo wa kweli ni lazima awe na sifa hizi 10 hapa chini.

  1. Kuzaliwa nchini na angalau mzazi mmoja au wote wawili wawe ni wazawa
  2. Kuona fahari yeye kuzaliwa nchini bila kuona aibu wala haya
  3. Ni lazima awe mwaminifu wa kulipa kodi, kutoibia nchi kwa njia yeyote.
  4. Kutokuwa mharibifu au mvujaji wa mali na rasilimali za nchi
  5. Kuwapenda watu wote, hata viongozi wanaoijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake.
  6. Kuwapiga vita na kuwapinga kwa nguvu zote raia wote wanaobomoa na kuharibu nchi hata kama ni wa chama chake, dini yake, kabila lake,  rangi  yake au ndugu na jamaa zake.
  7. Kusaidiana na viongozi wake kuijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake
  8. Kuweka juhudi kubwa katika kuisema na kuitangaza nchi yake vizuri ndani na nje ya mipaka yake.
  9. Kupenda vitu vinavyoihusu au kutoka au kutengenezwa nchini mwake kama lugha, utamaduni, vyakula, bidhaa za viwanda, timu za michezo, wana michezo wake, na kila kitu kizuri kinachotokana na nchi yake.
  10. Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu, majirani na marafiki kuwa wazalendo kwa kuipenda na kujitoa kwa ajili ya nchi yao.

MIFANO YA WAZALENDO WA KWELI

Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaweza kuwa mfano mzuri wa Mtanzania Mzalendo kwani anaingia katika sifa zote 10 hapo juu.

Edward Moringe Sokoine pia anawekwa kwenye orodha ya watanzania wazalendo ambao kwa kweli waliipigania hii nchi na watu wake na rasilimali zake hata na kupoteza maisha yake,

HITIMSHO

Kuwa mzalendo ni zaidi ya kuifia nchi yako. Kwa sababu aidha kwa uzembe au kwa ujinga au kwa imani yake mtu aweza kufa lakini kumbe hakuipenda nchi ila kwa matakwa yake binafsi. Shinikizo la kuifia nchi ni lazima liwe tunda la uaminifu, upendo kujitoa, kuipigania na kuitetea nchi yako. Wako wazalendo ambao wameitetea nchi yao toka utotoni, ujanani na uzeeni na hawakuifia nchi. Watu wasio wazalendo ni hawa hapa: watu wanaoihujumu nchi kwa kuiba, kutumia rasilimali za nchi viabaya, kuharibu miundo mbinu, kuweka pesa nje ya nchi, kuisema vibaya nchi na viongozi au watu wake, kushabikia wizi na ufisadi, kuvunja sheria za nchi, kuthamini vitu na mambo kutoka nje, nk.

Unaweza kweli ukawa Mzawa, mwaminifu, mkweli lakini unakuwa kimpya watu wanapoiba na kutumia vibaya rasilimali za nchi, wewe pia sio mzalendo kwa mfano huo.

SOMA ZAIDI

Nyimbo za kizalendo,

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi