Elimu au mafunzo ya masoko kwa wafanya biashara wadogo ni muhimu sana kwani hiki kipengele wengi huwa hawaifuati na matokeo yake biashara nyingi zinakufa au kudumaa.
Fuatilia makala hii na kama unaswali unaweza kutuandikia au kutoa maoni yako ili watembeleaji wengine wa haya makala wakushauri na kukupatia majibu
Majadiliano: Mwezeshaji na wawezeshwaji
Baadhi ya maswali muhimu kwenye mjadala ni
- Mfanyabiashara unauza wapi bidhaa yako au huduma yako?
- Unauza lini, taja majira au tarehe katika mwaka mzima?
- Je unauza nini, fafanua aina na maelezo ya kin a ya bidhaa/huduma yako unayouza ili ikupatie mapato
- Yataje pia mafanikio katika biashara yako angalau kwa miaka mitatu iliyopita
- Piua elezea changamoto mbalimbali ulizozipitia au kukutana nazo na njia ulizotumia kukabilinan nazo
- Nini maoni yako ya jumla kwa wafanya biashara wenzako au washiriki wa semina/warsha
Dhana ya masoko
Dhana kubwa inayotumika katika masoko ni hii ya Pyramid ambayo huelezea jinsi watu wanavyopungua katika kila ngazi ya kupand pyramid. Hii dhana imechukulia mzunguko wa masoko kwa mwezi mmoja
- Public – uma (hii ni namba ya watu utakaowafikia kwenye matangazo yako. Mfano umetolewa kwenye radio yenye uwezo wa kuwafikia watu milioni tatu (3m)
- Leads – Watu watakaofuatilia huduma yako- kwa mfano wa pyramid hapo juu tunategemea baada ya watu 3M kusikia tangazo la bidhaa/huduma yako, watu elfu hamsini watafuatilia kwa email, website, mitandao ya kijamii, simu na saa nyingine kuja ofisini
- Customers – Wateja (Hawa ni watu ambao utafanikiwa kuwashawishi kununua bidhaa/huduma yako na wakakubali. Kwa mfano hapo juu tunategemea watu 500 watakuja kununua bidhaa yako. Kuuza(selling) nitendo la kumshawishi leads, au watu wanaofuatilia huduma yako ili waamue kuja kununua. Kwa jina rasmi hii inaitwa kwa kimombo “Selling Transaction”
- Repeat customers – Wateja wanaorudi (Ukitoa huduma nzuri kwa wateja yaani customer care, wengi wao watarudi. Idadi ya watakaorudi itategemea sana na aina ya customer service utakayowapa wateja wako. Kwa mfano hapo juu tunategemea wateja 200 watakuwa wakirudi kila mwezi. Pia ukiongeza dhamani ya bidhaa na ukubwa na upana wa kukidhi mahitaji ya mteja utawashawishi wengi warudi
Taarifa za wateja (customer’s database)
- Weka taarifa za wateja yaani database yao yenye data hizi, Jina, simu, barua pepe, tovuti, shughuli yake na historia yake ya manunuzi
Hatua za kufuata katika kutekeleza utafutaji wa masoko
Unatakiwakufanyauchanganuziwasokoyaanimarketanalysis
- Kuinisha wateja wako – customer identification
- Kuanisha mahitaji yao – Need assessment
- Kuainisha uwezo wao wa kiuchumi – purchasing power
- Kujua idadi ya walengwa – market volume
- Kujua wanapatikanaje/wanafikiwaje – How to access them
- Kuainisha uwezo wako wa kuhudumia soko kwa maana ya mtaji, wafanyakazi, ujuzi, wanaokupa huduma nk – Analyse your ability to save the market in terms of capital, personel, skills and service providers etc
- Jifunge mkanda na uthubutu kutekeleza sawasawa na ulivyopanga- pull up your socks and try to do according to plan
Njia kuu za kuwafikia walengwa
- Radio
- TV
- Magazeti
- Mikutano/kongamano/warsha/semina
- Tovuti (website)
- Gari la matangazo
- Mabango
- Vipeperushi/vitabu/majarida/Makala/Kadi nk
- Kutembelea ofisini/nyumbani
Utekelezaji: Mpango mkakati na Kalenda ya kufanya masoko
- Anzan na majaribio ili kujifunza na kugundua madhaifu katika mipango na utekelezaji
Mpango mkakati
Weka mpango mkakati utakaoonyesha melengo pamoja na viashiria vya kupima mafanikio ya zoezi. Mfano katka mwezi huu wa masoko unategemea kuwafikia
- Wateja wangapi?
- Maeneo yepi?
- Kwa gharama ya kiasi gani
Andaa roadmap
Hii muhsasari wa ramani utakayotumia ili kuwafikia wateja wengi kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi. Usipoweka roadmap unaweza kuwafikia wateja lakini kwa gharama kubwa na kutumia muda mwingi
Kalenda ya masoko
Andaa kalenda itakayokuongoza jinsi gani utaanza na kuendelea kufanya kazi ya masoko
Kalenda ionyeshe yafuatayo
- Tarehe
- Shughuli,
- Kusudi
- Mahitaji
- Bajeti Mhusika
- Anza utekelezaji halisi kama majaribio imeonyesha mafanikio
Ufuatiliaji na tathmini
Ufuatiliaji
Ufuatiliaji ni utaratibu mzuri wa kuhakikisha unajua kama zoezi linaleta matokeo
Kwa jinsi rahisi ufuatiliaji unakuwa hivi
Kabla zoezi halijaanza kuwepo na rekodi yaidadi ya wateja wanaofuatilia huduma yako/yenu kupitia
- Simu
- Website
- Mitandao ya kijamii
- Kutembelea ofisini kuulizia huduma nk
Baada ya zoezi kuanza weka tena rekodi yako kama ilivyoelezwa hapo juu halafu linganisha,
Kulingana ni viashiria vyako ulivyoweka kwenye malengo yako uanweza sasa kujua kama kusudi linafikiwa, litafikiwa au la
Tathmini
Tathmini ni zoezi la kuanisha rekodi na repoti mbalimbali za masko kwa kutumia mtaalamu na kuanisha mapendekezo ya kuboresha zoezi la kufanya masoko kwa kuzingatia madhaifu yaliyoonekana wakati wa tathmini
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |