Neno ujasiriamali ilianza kutumika miaka ya 1700 likiwa na maana ya kawaida ya kuanzisha biashara.
Maana ya ujasiriamali Kutoka kwa Wachumi
Ujasiriamali ni Kukabiliana na vikwazo za biashara endapo kuna uwezekano wa kupata faida. Kwa wengine ni kuwa na uwezo wa kukwepa vikwazo za biashara ili ufanikishe biashara yenye faida.
Pia wengine wamemuelezea mjasiriamali kama ni mtu mbunifu mwenye uwezo wa kuuza ubunifu wake.
Wachumi wengine wameendelea kumuelezea mjasiamali kama mtu mwenye kuleta bidhaa au huduma za kibunifu kwenye soko ambazo hazijawahi kuwepo.
Katika karne ya 20, mchumi mmoja kwa jina Joseph Schumpeter (1883-1950) alifafanua kuwa mjasiriamali ni mtu mwenye kuleta ubunifu na maboresho yenye kuleta sio tu hamasa bali pia kuwa kichocheo cha mabadiliko.
Joseph Schumpeter aliendelea kumuelezea mjasiriamali kama “mbunifu mharibifu” maana yake ni kwa kuwepo wajasiriamali na bidhaa au huduma zake, viwanda huduma na au bidhaa dhaifu na za zamani zilikufa na kutoweka kabisa kwenye soko.
Wachumi wengi leo hii wanaamini kuwa Mjasiriamali ni moyo na kichocheo katika kukua kwa chumi za nchi mbalimbali duniani.
Maana ya ujasiriamali Kutoka kwa Wafanyabiashara
Mfanyabiashara mtaalamu, Peter Drucker (1909-2005) alielezea wazo hili kwa mapana mengine kuwa, mjasiriamali ni mtu anayepeleleza mabadiliko, kuwa na mwitikio wa haraka na kuhatamia fursa zilizopo katika mabadiliko. Mfano wa hili ni mabadiliko yaliyotokea katika sekta ya mawasiliano kutoka typriter kwenda kompyuta nk.
Mjasiriamali anaweza kutokea katika hali yeyote, msomi au sio msomi, mhandisi, mwanasheria au mwalimu mchungaji au shkhe nk.
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |