Biashara Binafsi

Jinsi ya Kuingiza Taarifa za Biashara Kwenye Website ya BRELA

UTANGULIZI

Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni na biashara kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua zifuatazo zinawawezesha wamiliki, wasimamizi wa makampuni na biashara kuingiza taarifa zao kwenye tovuti ya BRELA

Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Hatua #1: Taarifa za msajili, mmiliki au wamiliki wa biashara

 1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
 2. Simu ya kiganjani
 3. Barua pepe yaani email

Hatua #2: Taarifa za biashara

 1. Aina ya biashara mtu binafsi, washirika au shirika
 2. Jina la biashara

Hatua #3: Ofisi ya biashara (Business Location)

 1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
 2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
 3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)

Hatua #4: Shughuli za Biashara (Business Activities)

 • Taja shughuli za biashara kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification

Hatua #5: Taarifa za Wamiliki (Business Owner’s Information) pamoja na Akaunti ya Benki kama ipo

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #6: Taarifa za Akaunti ya Benki Zingine kama ipo (Business Bank Account Information)

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #7: Taarifa za Wawakilishi (Person who can update ORS Information)

 1. Aina ya mmiliki kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mmiliki kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu

Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)

Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-

 1. Consolidated form iliyosainiwa wamiliki wote wa biashara
 2. Viambatanisho vingine vinakuja

Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)

Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini

 1. Kusajili biashara = TZS. 15,000
 2. Kuhifadhi nyaraka na = TZS. 5,000/mwaka

Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)

Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni

 1. Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money na HaloPesa
 2. Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB

Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo.

HITIMISHO NA USHAURI

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka karatasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:

 1. Nashauri kama unataka kuingiziwa taarifa za biashara yako kwa haraka wasiliana nasi kwa mawasiliano
 2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
 4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za kampuni au biashara chapu chapu tafadhali wasiliana namikupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Gharama za usajili wa kampuni BRELA kwa ufupi ni

Hatua saba (7) muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara

 1. Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
 2. Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
 3. Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao  – siku ya tatu
 4. Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
 5. BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
 6. Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho.  Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
 7. Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF

Kumb:

 1. Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
 2. Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
 3. Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
 4. Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
 5. Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.

MZUNGUKO WA MCHAKATO WA KUSAJILI KAMPUNI BRELA

Maelezo zaidi ya namna ya kusajili biashara au kampuni BRELA

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi