Default Logo Image for BRELA Online Registration System

Hatua 10 Rahisi za Kusajili Kampuni Kupitia Website ya BRELA

UTANGULIZI

Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BREAL. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana namikupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI

Hatua #1: Taarifa za msajili

Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la  kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).

Taarifa zenyewe ni:-

 1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
 2. Simu ya kiganjani
 3. Barua pepe yaani email

Hatua #2:  Taarifa za kampuni

Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-

 1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
 2. Jina la kampuni
 3. Tarehe ya kufunga mahesabu – mfano 31 Desemba
 4. Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically

Hatua #3:  Ofisi za kampuni

Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-

 1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
 2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
 3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
 4. Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Mfano wa anuani ya makazi yasiyopimwa
 1. Region: Arusha
 2. District: Arusha CBD
 3. Ward: Unga Limited
 4. Postal: code 23107
 5. Mtaa: Viwandani,
 6. Kitongoji: Olevolosi
 7. Karibu na kiwanda cha ATOZ
Mfano wa anuani ya makazi yaliyopimwa
 1. Region: Arusha
 2. District: Arusha CBD
 3. Ward: Kati
 4. Postal code: 23102
 5. Street: New Livingstone Street
 6. Road: New Livingstone Road
 7. Plot number: 91
 8. Block number: F
 9. House number: 704

Hatua #4:  Shughuli za Kampuni

 • Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification

Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi

Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-

 1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. TIN
 5. Simu ya kiganjani
 6. Barua pepe yaani email
 7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
 8. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email

Hatua #6:  Taarifa za katibu wa kampuni

Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-

 1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. Simu
 5. Barua pepe – email
 6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
 7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)

Hatua #7:  Taarifa za wanachama/wenye hisa

Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-

 1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
 2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
 3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
 4. Simu
 5. Barua pepe – email
 6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
  1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
   1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
   2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
   3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
 7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
 8. Thamani ya hisa za mtaji mfano mil 20
 9. Mgawanyo wa hisa kwa wanachama kwa namba au asilimia( mfano hisa za Mil. 20M halafu mwenye hisa wa kwanaza 60% na wa pili 40%= mgawanyo utakuwa hivi. Asume kila hisa itakuwa na thamani ya 100,000 na kwa hiza za Mil 20 utakuwa na jumla ya hisa 200, wa kwanza atapata hisa 120 (60%) na wa pili atapata hisa 80 (40%))

Hatua #8:  Viambatanisho

Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-

 1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
 2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
 3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
 4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni

Hatua #9:  Ada za usajili na kufaili

Malipo ya ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini

 1. Kusajili kampuni
 2. Kuhifadhi nyaraka na
 3. Stamp Duty

Hatua #10:  Namna ya kulipa ada

Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni

 1. Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa
 2. Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB

Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

HITIMISHO NA USHAURI

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi magumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia.

Nashauri yafuatayo:

 1. Nashauri kama unataka kufanya usajili wa haraka na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia.
 2. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho.
 3. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana namikupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu wa mawasiliano

Gharama za usajili wa kampuni BRELA kwa ufupi ni

Hatua saba (7) muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara

 1. Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
 2. Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
 3. Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao  – siku ya tatu
 4. Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
 5. BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
 6. Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho.  Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
 7. Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF

Kumb:

 1. Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
 2. Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
 3. Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
 4. Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
 5. Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.

MZUNGUKO WA MCHAKATO WA KUSAJILI KAMPUNI BRELA

Maelezo zaidi ya namna ya kusajili biashara au kampuni BRELA

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi