Hii ni aina ya mkate ambao unakaa kama mfuko na unaweza kujaza na matunda, mbogamboga au wakati mwingine nyama. Mkate huu pia unaitwa mfuko wa pita

Kuna hatua mbili kuu za kutengeneza mkate wa pita

1.      Kutengeneza mfuko wa pita au mkate wenyewe

Mahitaji: kwa watu 2-4

  • Unga wa ngano ½ kilo
  • Amira kijiko 1 ½
  • Chumvi ½ kijiko
  • Maji ya vuguvugu kikombe 1
  • Mafuta ya kupikia kijiko 1 ½
  • Asali vijiko 2
  • Sukari kijiko 1

Hatua za kufuata ili kuandaa mifuko ya mkate wa pita:

  • Chekecha unga wako ili kuingiza hewa kwenye unga
  • Weka amira, chumvi, sukari kisha changanya
  • Weka asali na mafuta ya kupikia kisha changanya
  • Weka maji ya vuguvugu na kisha kanda unga huo mpaka ulainike
  • Katakata na kisha tengeneza vichapati vidogo na vyembamba
  • Weka vichapati hivyo jikoni moto usiwe mkali sana
  • Pika vichapati hivyo mpaka viive ila visiungue
  • Acha chapati hizo zipoe
  • Kata vichapati hivo nusu kwa nusu

2.      Kujaza mkate wa pita

Kujaza mkate wa pita inategemea na matamanio yako au kitu unachotaka kuweka kwenye mfuko wa pita.

Mfano : nyama ya kusaga na kachumbari ya nyanya

Mahitaji ya vijazo:

  • Nyanya 2 kubwa
  • Vitunguu 2 vikubwa
  • Pilipili manga kijiko 1 ½
  • Chumvi kijiko 1 kidogo
  • Tangawizi vijiko 2 vidogo
  • Nyama ya kusaga ½ kilo
  • Limao 1 dogo
  • Mafuta ¼ kikombe

Hatua za kupika na kuaandaa vijazo vya mkate wa pita:

  • Chukua nyama ya kusaga kisha changanya na pilipilimanga, chumvi, tangawizi kisha iache kwa dakika tano
  • Osha, menya na katakata vitunguu kisha visugue na chumvi kuondoa ukakasi
  • Osha, katakata nyanya viwe vya mviringo
  • Changanya nyanya, vittunguu, chumvi, limao na pilipilimanga ilki kutengeneza kachumbari
  • Chukua nyama yako ya kusaga na kaanga/pika na mafuta mpaka iive

Kwa kumalizia:

  • Chukua mifuko ya pita na kisha anza kujaza na nyama ya kusaga na kachumbari yako
  • Ukitaka unaweza kuongezea sauce au mayonise au pia tomato

 

Asante na karibu