Elimu ya Awali kwa Watoto Wetu

Umuhimu wa Elimu ya Awali (Chekechea) kwa Watoto Wetu

UTANGULIZI

Chekechea ni mjuhimu pengine hata kuliko msingi kwa sababu ya mambo yanayofundishwa huko inamfanya mtoto aweze kujitambua na kuyapenda mazingira yake kwa kiwango cha juu. Inamfanya awe mtoto anayewajibika na elimu. Elimu hii ya awali ni sawa na michoro ya nyumba kabla ya kuweka msingi. Uchoraji ukiwa mbaya na msingi ano uatawekwa vibaya.

Kuna watu wanadai huu ni wajibu wa wazazi na napenda kusema kwamba wazazi hawataweza kuwapa elimu ya awali watoto wao nyumbani kwa sababu ya kiwango cha nufahamu wa jambo hili na pia wazazi wengi  wako busy na kutafuta pesa.

Changamoto kubwa hapa ni waina ya waalimu wanaowekwa kuwafunza watoto katika umri huo na pia sera za nchi kwenyue hili eneo, wengine huwalea vizuri na wengine kuwapandikiza sumu ya mtoto kuchukia shule.

FAIDA YA ELIMU YA AWALI KWA WATOTO

Ukiangalia kwa juu juu utaona kama hakuna tofauti ya wasomi wa kale ambao hawakusoma shule za awali au chekechea na wasomi wa sasa walienda chekechea lakini mimi nasema kuna tofauti kubwa. Kuna tofauti kubwa ya IQ ya watoto walio hudhuria shule za awali na wale ambao hawakufanya hivyo . Tofauti haijitokezi kwa mtu mmoja mmoja, bali inajitokeza kwa kundi kubwa la sample.

Kuna tafiti zilizofanyika huko nyuma ya kuhusisha mchango wa elimu kwenye IQ na ikagundulika kuwa jinsi mtoto anavyokuwa darasani IQ yake inakuwa kubwa kuliko akiwa nje ya darasa. Hata kwa vijana wa vyuo pia utafiti ulionyesha hivyo hivyo kuwa viijana walio chuoni IQ yao ni kubwa kuliko wale ambao wako tu mtaani.

Ingewezekana kumpeleka mtoto shule akiwa tumboni ningeshauri hivyo ila haiwezekani.

Tafiti zilizofanywa na Cambridge University huko nyuma zinaonyesha kuwa mtoto akiwa tumboni akasemeshwa na kuulizwa maswali na mama yake IQ yake inakuwa kubwa tofauti na wale watoto ambao mama zao huwa hawawasemeshi wakiwa tumboni.

Vivyo hivyo mtoto akizaliwa elimu ya awali inatakiwa ianze maramoja ili kuendeleza IQ ya mtoto isipungue.

MAONI NA HITIMISHO

Kwa hiyo mimi nahitimisha kwa kushauri kuwa awe ni mama au baba au mwalimu anatakiwa kumfundisha mtoto, mtoto akiwa kwenye umri wowote anatakiwa awe anapewa elimu kulingana na umri wake ili kuinua IQ yake na hivyo kuongeza kasi ya ubongo wake kwenye kuhifadhi, kuchambua, kugundua na kufanya maamuzi sahihi na ya haraka akiwa mtu mzima.

VYANZO VYA KUREJEA

  1. IQ Test Experts
  2. Early Childhood Development – World Bank
  3. Benefits of Early Childhood Education – parents.education.govt.nz
  4. Proven Benefits of Early Childhood Interventions – rand.org

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi