Register
A password will be e-mailed to you.

Uandishi wa ripoti unategemea sana mambo kadha wa kadha kama ilivyoorodheshwa hapa chini:

Ripoti hiyo ni ya aina gani

 1. Ya Kesi?
 2. Ya Utendaji kazi wa kawaida?
 3. Ya Utafiti?
 4. Ya kuanzisha mradi?
 5. Ya shule/chuo
 6. Ya cheo kipi? Afisa, meneja, mkurugenzi
 7. Kwenda kwa nani, afisa, mkurugenzi, bodi nk

Maswali yanaendelea na majibu yake ndio msingi muhimu wa uandishi wa ripoti

Pamoja na hayo yote, mfumo wa ripoti karibu unafanan kwa maeneo muhimu hapa chini:

Mfano ripoti ya Mei 2015

 

 1. Utangulizi
 2. Malengo (Lengo kuu na malengo Mahsusi)
 3. Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa Mei 2015
 4. Kazi zilizotekelezwa kiwango cha utekelezaji na majadiliano yake (Hapa elezea kwa takwimu na au viashiria, takwimu kama unaripooti matokeo yanayohesabika au viashiria kama unaripoti matokeo yasiyohesabika)
 5. Kiambatanisho cha ripoti ya fedha(Hiki kipengele ni muhimu kama unasimamia fedha au utendaji wako ulihusisha matumizi ya fedha)
 6. Kazi zilizofanywa ambazo hazikuwepo kwenye mpango (elezea kama hapo juu)
 7. Habari njema
 8. Changamoto na njia za kutatua
 9. Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa June 2015
 10. HitimishoLeave a Reply