Watoto wakijifunza Kupiga Gitaa
Kujifunza kupiga gitaa ni mojawapo ya stadi za maisha kwa mtoto/kijana

Stadi za Maisha kwa Mtoto/Kijana

stadi za maisha kwa watotoStadi za Maisha ni ujuzi ambao sio rahisi watoto au vijana wapate kupitia mitaala ya kawaida darasani au vyuoni. Ni ujuzi wa asili ambao mtoto au kijana anaupata katika mazingira yake ya asili (Hapo anapoishi).

Ni familia chache sana ambazo zimekuwa zikiwafundisha ujuzi huu watoto wao na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya mafanikio huku familia nyingi hasa za wasomi zikiwasisitizia watoto wao elimu tu kama ndio njia kuu ya kufanikiwa kimaisha.

Ili mtoto au kijana wako aweze kufanikiwa katika kujifunza stadi za maisha, umuandae kiakili, kiroho na kisaikolojia. Mzoeshe namna na njia rahisi za kutumia muda wake kwa busara bila kuupoteza kiholela kwa mambo yasiyo muhimu na yasiyopangwa. Muongoze kuachana na marafiki wasiofaa, tabia zisizofaa, daima awe na mtizamo chanya kwenye maisha. Mtizamo wa kufanikiwa, kuweza. Mtoe kwenye mitizamo ya kidunia ambayo huweka mbele matukio ya kupoteza muda kama mitandao ya kijamii, kujipodoa kwa watoto wa kike, kushinda kwenye TV labda kama anajifunza nk

Elimu ya stadi za maisha kwa watoto na vijana hutofautiana kulingana na:

  1. Umri
  2. Eneo au mazingira.

Hivyo mafunzo haya yasingatie hivyo vigezo viwili hapo juu.

Kama unamtakia mtoto/kijana wako maisha bora na yenye mafanikio ya baadaye mfundishe au muelekeze stadi za maisha zifuatazo:

  1. Mfundishe mwanao namna ya kuandaa bajeti ya pale nyumbani kwako kwa kutumia karatasi na au kompyuta
  2. Mzoeshe mwanao kulipa bili mbali mbali kama za TV, tanesco, maji nk
  3. Mzoeshe mwanao kufanya manunuzi sokoni na supermarket
  4. Mzoeshe mwanao kurekebisha/kutatua matatizo madogomadogo ya pale nyumbani kama ya umeme, maji, TV, vitasa vya nyumba, rangi,  nk
  5. Nenda naye kazini kwako hasa wakati wa likizo na kumfundisha kazi zako taratibu kama fursa inaruhusu mfano namna ya kupiga simu za kiofisi, namna ya kuandika na kutuma email, namna ya kutuma na kupokea faksi, namna ya kuprint na kutoa photocopy, namna ya kuscan, namna ya kuafail na kutoa barua kwenye mafail  (badala ya kumpeleka tuition)
  6. Mzoeshe utoaji mfano kanisani mpe sadaka akatoe yeye kwa niaba yako au mpe sadaka kama yako. wewe ukitoa 5,000 na yeye mpe elfu tano kama huna basi wewe baki mpe mtoto akatoe kwa niaba yako. Mzoeshe pia kutoa kwa maskini na wenye uhitaji. Usimzoeshe mtoto kutoa sadaka za kitoto kama mia moja nk. Atazoea kutoa kidonjo hata akiwa mkubwa.
  7. Mzoeshe kuwaombea wadogo zake, wakubwa zake, majirani, eneo mnaloishi, nchi, viongozi, marafiki na maadui kama wapo.
  8. Mfundishe na umzoeshe kufanya biashara ndogo ndogo pale nyumbani (kulingana na umri wake)
  9. Mzoeshe kuongoza ibada ya nyumbani na kufanya maombi
  10. Mzoeshe kwenda kusalimia marafiki na majirani wa karibu (close friends and relatives)
  11. Mzoeshe mwanao pia kuwatembelea watu walio kwenye shida mfano kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, wafungwa magerezani na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwenye vituo vya kulelea watoto yatima nk.
  12. Mzoeshe kusema samahani anapokosea na asante anapofanyiwa wema na kusema nimekusamehe anapoombwa msamaha
  13. Mzoeshe kusifia mwenzake hasa wadogo zake au wakubwa zake pale wanapofanya vizuri hata kama ni kwa haba
  14. Mzoeshe kuwa mdadisi wa mambo (critical thinker) Mfano kwani ukirusha kitu juu inarudi chini, kwa nini mchana kuna mwanga na usiku kuna giza? kwa nini tunakula? kwa nini anasoma? na maswali mengi ya kimaisha
  15. Mzoeshe mtoto wako kufanya jambo jipya kila siku au jambo lilelile kwa namna mpya (to be creative and innovative)
  16. Mzoeshe mtoto kusoma (mfano vitabu, magazeti, majarida yenye kuelimisha)
  17. Mzoeshe mtoto kutambua vipawa na vitu anavyovipenda kufanya ili aviendeleze
  18. Mzoeshe mtoto kupenda wenzake kwa matendo. (mfano kumwomba Mungu amuwezeshe kupenda wengine, kuwaombea wengine wapate mafanikio kwa Mungu, kuwapa zawadi wadogo zake na wakubwa zake -akinuanua pipi mbili, moja yake na moja ya rafiki yake au mdogo wake au mkubwa wake)
  19. Mfundishe mtoto wako mambo kadha wa kadha ya kimaisha kama vile uongozi, usimamizi wa fedha, biashara na ujasiriamali, namna ya kufanikiwa katika masomo, namna ya kuweka vipaumbele, namna ya kuhusiana na wenzake, namna ya kutatua migogoro yanapotokea, namna ya kufanya maamuzi hasa maamuzi magumu. nk
  20. Jizoeshe kutoka out kama za lunch, kutembea, shopping na mtoto wako na kutumia huo muda kumfundisha mambo kadha kadha ya kimaisha. Hii inategemea out hiyo ni ya wapi na ya kusudi lipi. Utakachomfundisha mtoto wako kiendane na mazingira yaani out destination na umri wake
  21. Jizoeshe kupumzika na mtoto wako na kufanya yale mambo mtoto anafanya (mfano kuangalia TV pamoja, kuangalia mechi za mpira pamoja, kucheza nk. kwenda kutembea pamoja ili uweze kumjua mtoto wako na anapendelea mambo gani na pia upate fursa ya kumuelekeza kwenye mambo yanayofaa zaidi). Tumia pia muda huu kumfundisha mtoto wako mambo kadha wa kadha ya kimaisha
  22. Jizoeshe kumkumbatia mtoto wako hasa mnaposalimiana au kushangilia jambo, au unapoelezea hisia zako za furaha kwake ili uimarishe mahusiano yako kwake na pia ujue kama yuko salama ili pale anapokuwa sio salama uwe wa kwanza kumtambua na kuonyesha upendo wako kwake kwa kumhudumia na kumpa maneno ya faraja. Watoto wengi wana tabia ya kuficha matatizo walizo nazo kama wazazi hawako karibu nao, mfano ana kidonda, ametendewa mabaya na wenzake au watu wabaya, ugonjwa wa ngozi, na magonjwa mengine. Unapokuwa na mazoea ya kumkumbatia mtoto wako utagundua mambo hayo. Mfano, kwenye kijiji kimoja hapo mwaka 1998 tulimtembelea mtoto mmoja katika na katika hali ile ya kumkumabtia tukagundua kuwa aliungua mgongoni na kwa hiyo tukafanya utaratibu wa haraka wa kumpeleka kwenye zahanati ya karibu akatibiwe kidonda kwani kilianza kuoza. Mfano mwingine: Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa tangu utoto wake hakuwahi kuwa karibu na baba yake kwani alikuwa mkali sana na siku moja walikubaliana na mama kumpiga kwa kosa ambalo hakulitenda. Kuanzia hapo akawa mbali na wazazi wake mpaka alipohitimu chuo kikuu. Hata adhabu tunazowapa watoto ziwe za kistaarabu. mfano umshirikishe mtoto kwenye adhabu yeyote unayotaka kumpa. Umsikilize vya kutosha kabla ya kumpa adhabu yeyote. Hata kama adhabu ni kali, mtoto akishirikishwa na kuridhika kwamba alistahili kuadhibiwa hataweka uhusiano wake na mzazi mbali.
  23. Fanya matukio kama ya birthday pamoja na mtoto wako huku akiwaalika marafiki zake wa karibu (hii itakuwa fursa yako ya kuwafahamu marafiki wa mtoto wako) mfano waweza weka kwenye electronik kalenda yako ikukumbushe birthday za watoto wako ili wewe ndie uwe mkumbushaji na kuhakikisha tukio hilo linafanyika. Kumbuka aina ya marafiki wa mtoto wako ndio watakaoamua mtoto wako aweje mbeleni na afanikiweje? awe na tabia za namna gani? nk
  24. Mzoeshe mtoto ajifunze kuwasikiliza wengine kwanza sio yeye tu asikilizwe tena kwa kumwangalia msemaji usoni na kujifunza kutumia luigha ya mwili kuwasiliana.
  25. Unapombeba mtoto wako kwenye gari muelekeze mambo kadha wa kadha mfano kuwasha gari, kuzima, kushika mbreki, kutumia usukani nk)
  26. Mzoeshe mtoto kuweka kumbukumbu kwa kuandika na jinsi ya kutunza mafaili yake kwa mpangilio sahihi, mfano matokeo yake yawe kwenye faili la kwake ambalo yeye mwenye analisimamia.
  27. Mzoeshe mtoto namna ya kutengeneza ratiba na kuifuata mfano ratiba ya siku, kuamaka, kufanya usafi, kwenda shule, kujisomea, kufanya homework, kufanya kazi za nyumbani, kucheza kuangalia vipindi maalum za TV au kanda nk.
  28. Mtoto ajizoeshe kuandika maono na malengo ya maisha yake ya muda mfupi, kati na mrefu
  29. Mzoeshe mtoto kutumia usafiri wa umma kama daladala.
  30. Mzoeshe mtoto kuwasiliana naye kwa barua ili azoee kuandika barua nzuri mfano za maombi ya vitu vinavyotakiwa shuleni na bei yake.
  31. Mzoeshe pia mtoto kufanya window shopping kwa vitu vya shuleni na zile za nyumbani kama vyakula na vifaa vingine vya nyumbani ili ajifunze naman ya kufanya manunuzi kwa dhamani halisi ya pesa (value for money).
  32. Mzoeshe mtoto kutumia kompyuta kwa matumizi madogo madogo kama ya kuanda bajeti kwa excel na kuandika maombi kwa MS Word
  33. Mzoeshe mtoto kuogelea hasa kwa wale walio karibu na mito, maziwa na bahari
  34. Kama hali ikiruhusu fanya utalii wa ndani na mtoto wako kama kutembelea mbuga za wanyama (kwa walio karibu na mbuga hizo) kutembelea matukio ya kimila, kutembelea zoo ya wanyama nk.
  35. Mnunulie mtoto kamera ndogo ya kujifunzia na awe anatumia kwenye matukio muhimu makanisani, shuleni nk
  36. Mzoeshe mtoto kutumia vifaa vya teknolojia kama simu an kompyuta katika kuwasiliana kwa message, email na sauti
  37. Mzoeshe na umuhimize mtoto/kijana wako kuandika makala, vitabu, historia ya maisha yake. Kwenye mada mfano aandike mambo yanayosaidia jamii kama usafi, upishi, ufundi, nk
  • Mambo haya haya wezekani ndani ya muda mfupi na inategemea pia na umri wa mtoto wako na mahali mnapoishi.
  • Vipengele vingine havihusiki na wewe kulingana na mazingira yako ya kuishi na umri wa mtoto wako
  • Pia kuna mambo mengi katika maisha mfundishe mwanao asijihusishe nayo kabla ya wakati wake. mfano mitandao ya kijamii, makundi ya marafiki wasiofaa/wasiojenga maadili, ulevi, urembo na kujiremba kwa kujipodoa au cosmetic beauty, mahusiano ya kingono au kimapenzi nk. Haya mambo mfano wa urembo na kujipodoa inaweza ikamfanya mtoto atumie muda wake mwingi kwenye kuwazia hayo mambo na kuyafanya kipaumbele katika maisha yake. Mtoto au kijana asiyejihusisha na mambo hayo akili yake na fikra zake kwa asilimia kubwa zitakuwa kwenye mambo ya kuijenga taaluma yake akiwa mkubwa kama haya mambo ya stadi za maisha na masomo darasani

 

Life Skills for Children WorkshopLife Skills for Children Workshop
Life Skills for Children Workshop provided to schools and local communities

 

Life Skills for ChildrenLife Skills for Children
A non-physical personal safety and communications course for children designed to improve confidence, self esteem, awareness personal safety and social interaction skills.

 

Kelly Bear Helps Elementary Children with Life Skills & Violence Prevention (Overview)Kelly Bear Helps Elementary Children with Life Skills & Violence Prevention (Overview)
Introducing Kelly Bear DVDs, featuring a life-size green bear named Kelly, who serves as a role model and teacher to five curious children. In the Violence Prevention DVDs Kelly helps children deal with bullying, resolve disputes, and use self-control. The Life Skills Education series teaches about self-understanding, personal safety, secret touching, friendship skills, problem solving, anger management, and positive behaviors. The programs are for children ages 3 to 9. Go to www.kellybear.com for more details.

Shua Life Skills Breaking the Bullying Circle Children's School Assembly ProgramShua Life Skills Breaking the Bullying Circle Children’s School Assembly Program
Ron Shuali of Shua Life Skills teaches children grade 1-5 effective ways to: Choose to stop being a bully Stop being a victim of bullying Get help as a bystander without feeling like it is tattling

 Life Skills for Kids: Equipping Your Child for the Real World …

A book I will be reffering to for the rest of my parenting years.” – Jonni McCoy, Miserly Moms. From the Inside Flap. Does your child know how to use a check

Parenting Secrets – Good Life Skills For Kids 5-12
http://www.raiseyourkidsright.com/
Respectful, responsible, hard-working kids who even do more than their share. Parenting tips by Mother of Five.

Busy Kids = Happy Mom: Life Skills
http://www.busykidshappymom.org/p/life-skills.html
Do not assume that your child has failed if they are behind. Children learn best by working alongside you. Printable list of all age 2-18 Life Skills located here.

Life Skills Every Child Needs – NYTimes.com

Apr 29, 2010 Ellen Galinsky’s latest book, “Mind In The Making.” It may well be the next iconic parenting manual.

Life Skills | Information Center | Education.com
http://www.education.com/topic/life-skills/
Welcome to our Life Skills resource center, stocked with practical toolkits for everyday life. Our goal is to help prepare your children for independence. Look here

Life Skills for Kids 2-18

Life Skills for Kids 2-18. Welcome & thank you for pinning to this board which focus on “Specific life skills that children should acquire before leaving their

Life Skills for Kids!
http://www.goodsitesforkids.org/LifeSkills.htm
A collection of great life skills educational sites for kids, children, teachers, and parents.

 

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi