Jinsi ya kupika pilau ya Nyama

Hatua na Jinsi Rahisi ya Kupika Pilau ya Nyama Tamu Sana

Aina za Pilau

  1. Pilau Nyama
  2. Pilau Bubu
  3. Pilau Maua
  4. Pilau Nyanya

Aina ya pilau kwenye andiko hili ni PILAU NYAMA

Chakula hiki ni kwa jili ya familia ndogo ya watu watano (walaji 5) 

Kabla hujaanza kupika chakula hiki ni vyema kuandaa vitu muhimu vitakavyohitajika kwen ye zoezi la kupika.

Hatua ya kuorodha ya viungo

  1. Mchele kilo1 ¼ 
  2. Nyama kilo ½
  3. Mafuta yakupikia lita ¼
  4. Njegere kilo ½
  5. Giligilani pakti ndogo 1
  6. Mdalasini ya unga packti ndogo 2
  7. Jira packti ndogo 2
  8. Chumvi packti ndogo 1
  9. Vitunguu-maji kubwa 3
  10. Vitunguu-saumu kubwa 1

Hatua ya kutayarisha viungo

  1. Ukisha andaa vitu vyote hivi tunaanza kuandaa chakula chetu cha Leo  
  2. Anza kumenya vitunguu saumu
  3. Katakata vitunguu maji
  4. Chambua girigilan
  5. Kata kata nyama
  6. Chukua vitunguu swaumu, girigilan, jira viweke kwenye kiuri na utwange vizuri hadi vilainike

Hatua na maelekezo ya kupika

  1. Chukua sufuria yako bandika jikoni weka mafuta
  2. Weka vitunguu maji jikoni
  3. Kaanga hadi viwe na ranging ya kahawia
  4. Weka nyama anza kuikaanga
  5. Endelea kugeuza nyama yako ikaange vizuri hadi iive  
  6. Chukua mchanganyiko wa vitunguu swaumu, girigilan, jira ulio twanga viweke na endelea kukaanga
  7. Chukua mdalasin weka koroga vizuri
  8. Weka chumvi geuza
  9. Weka njegere zako geuza vizuri ichanganyike
  10. Weka maji acha ichemke kwa dakika tano
  11. Weka mchele geuza vizuri taraaraatibu
  12. Funika na uweka moto mdogo wakuivisha chakula taratibu kwa dakika kumi
  13. Funua chakula chako geuza hapo kitakua pilau iliyo tayari  kwa kula  

Hitimisho na Mawasiliano ya Mwandishi

Kwa kuhitimisha napenda kusema tu kwamba upishi wa pilau uko wa aina nyingi na hata ndani ya aina moja bado mapishi yanaweza kutofautiana sana na inategemea Zaidi ubunifu wa mpisha kuweza kupindisha pindisha baadhi ya taratibu ili kuweza kupata chakula kizuri, kitamu na kinachowavutia walaji na hata wapiti njia

Mfano tu kwenye pilau ya nyama unaweza weka nyama nyingi, kawaida au chache, unaweza kubadilisha rangi ikawa kahawia au njano nk

Kwa wale walioko Arusha na wanahitaji huduma hii mnaweza kunipigia kupitia Simu kwa maelezo Zaidi,

  • Jina: Elizabeth Martin
  • Blog: https://www.kivuyo.com
  • Simu: 0674665279

ASANTENI SANA KWA KUSOMA ANDIKO LANGU NA KARIBUNI SANA KWA MAONI

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi