Register

2 × five =

A password will be e-mailed to you.

Kuandika dondoo za mkutano ni kazi rahisi kama kuna maandalizi ya kutosha lakini pia ni kazi ngumu kama hakuna maandalizi bayana kabla ya mkutano.

Maandalizi kabla ya mkutano

 1. Hakikisha sehemu ya ukumbi wa mkutano una nyenzo zote wezeshi kwa ajili ya kuchukua dondoo
 2. Vifaa vyote vya kuchukulia dondoo zimewekwa tayari na zinafanya kazi kama vile kalamu, karatasi, computer/laptop, jenerata kama utatumia vifaa vinavyotumia umeme, kifaa cha kurekodi kama utaamua kurekodi, kamera, nk
 3. Tayarisha ajenda za mkutano na katika mfumo wa ripoti ya mkutano ikiwa ni pamoja na maazimio yaliyotekelezwa au yaliyohitaji kutekelezwa kutoka kwenye mkutano uliopita

Wakati wa mkutano

 1. Andaa karatasi au mfumo wa kusajili wajumbe
 2. Hakikisha unawatambua wajumbe wa mkutano kwa majina yao
 3. Andika muda mkutano umeanza (Utahitaji kwa ajili ya ripoti ya mkutano)
 4. Usiandike kila kinachojadiliwa lakini hakikisha unaandika kila kilichoazimiwa
 5. Kama maazimio yanahitaji mlolongo wa utekelezaji kama watu/timu, muda na mahitaji mengine andika yote hayo
 6. Andika muda mkutano umefungwa (utahitaji pia hii kwenye ripoti ya mkutano)

Baada ya mkutano

 1. Andika rasimu ya ripoti haraka wakati ammbo bado unayakumbuka na kama kuna vitu vinakuchanganya waulize baadhi ya wajumbe waliokuwepo
 2. Zingatia mfumo wa uandikaji wa ripoti
 3. Soma ripoti yote na umpe mjumbe wa karibu naye asome na kukosoa kabla ya kutuma
 4. Tuma ripoti kwa mwenyekiti au mhusika mwingine wa mkutano

 

 Mfano wa dondoo za mkutano

 

English Form

Fomu ya Kiswahili


About The Author

Lemburis Kivuyo is a Busi­ness, IT and Com­mu­nity Related Project Consultant. Specialized in Business Establishment, Leadership training, Online Marketing, Small groups and teams leadership and management, Curriculum Development, Constitution development and much more.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.

fifteen + seventeen =

PO Box 1999, city, country
SLP 1999, mji, nchi