Ifuatayo hapa chini ni mfano wa uandishi wa dondoo za mkutano au kikao chochote. Maoni ya namna ya kuboresha yanakaribishwa
Maelezo ya ziada
- TDG = Kifupi cha Tumaini Development Group
- 5 = mkutano wa 5
- namba ya mwisho ya 1-10 ni namba ya agenda
- Ajenda namba 1, 2, 8, 9, 10 ni agenda za lazima kwenye kikao chochote
- Namba 8, 9 na 10 zinaweza kutofautiana lakina kichwa cha ajenda itakuwa ni ile ile
Tumaini Development Group
SLP 12908, Arusha
Taarifa ya Mkutano wa 5 wa Kikundi cha Tumaini uliofanyika Arusha Hall Tarehe 12/4/2012
Waliohudhuria
- Juma Hamad – Mwenyekiti
- Mary John – Katibu
- Kyuga Mwasige – Mjumbe
- Mwakagenda Samsoni – Mjumbe
- Mwanaidi Hamisi – Mjumbe
- Orodha ya waliohudhuria inaendelea jina moja kwa mstari mmoja
Walioalikwa
- Lomayani Loitore – Mwanasheria
- Jackson Mwita – Mshauri wa mikopo CRDB
- Orodha ya waalikwa inaendelea jina moja kwa mstari mmoja
Wasiohudhuria
- Henry Mambo – Ametoa sababu
- Jaffar Haji
- Orodha ya wasiohudhuria inaendelea jina moja kwa mstari mmoja
Ajenda
- Kufungua mkutano
- Kuthibitisha dondoo za mutano uliopita
- Kujadili yatokanayo na mkutano uliopita
- Mkopo wa CRDB – mpya
- Mkatabawa mradi wa maji – mpya
- Mikopo kwa wanachama – mpya
- ………………………….-mpya
- Mengineyo (AOB) (Kwa idhini ya mwenyekiti)
- Kuweka tarehe ya mkutano ujao
- Kufunga mkutano
TDG5-1: Kufungua mkutano
Mkutano ulifunguliwa tarehe 12/4/2012 saa 4:20 asubuhi na mwenyekiti
TDG5-2: Ajenda Zilizopitishwa
- Kufungua mkutano
- Kuthibitisha dondoo za mutano uliopita
- Kujadili yatokanayo na mkutano uliopita
- Mkopo wa CRDB– mpya
- Mkatabawa mradi wa maji– mpya
- Mikopo kwa wanachama– mpya
- ………………………….-mpya –imeahirishwa kujadiliwa mpaka kikao kijacho
- Mengineyo(Kwa idhini ya mwenyekiti)
- Kupokea wanachama wapya
- Kuweka tarehe ya mkutano ujao
- Kufunga mkutano
TDG5-3: Kusoma na kuthibitisha dondoo za mkutano uliopita
Dondoo za mkutano wa nne zilisomwa na kuthibitishwa na wajumbe
TDG5-4: Yatokanayo
Yafuatayo ni yatokanayo na mkutano uliopita, Maelezo zaidi kiambatanisho na. 1
- Katiba ya TDG
Imeazimiwa kwamba kamati ay katiba inayoongozwa na Lesom iwakilkishe rasimu ya katiba kwenye mkutano ujao
- Taarifa za fedha
Mkutano umeazimia kuwa marekebisho yote yaliyopendekezwa yafanyiwe kazi kabla ya mkutano ujao
TDG5-5: Mkopo wa CRDB
Mkutano umeazimia kuwa Mtunza hazina na wajumbe wawili wa mkutano wafuatilie na kujaza fomu za mkopo na kuwakilisha kwa mwenyekiti kwa ajili ya kuchukuliwa maamuzi kwenye mkutano ujao
TDG5-6: Mkataba wa mradi wa maji
Mkutano umeazimia kuwa kamati ndogo ya maji isome mkataba wa mradi wa maji kwa kushirikiana na mwanasheria na kuleta ripoti kwenye mkutano ujao
TDG5-7: Mikopo kwa wanachama
Imeazimiwa kuwa wanachama wanaotaka mkopo wa kujenga nyumba na wanakidhi masharti yote wapewe mikopo bila kuzungushwa.
TDG5-8: Mengineyo
- Kupokea wanachama wapya
Mkutano umeazimia kuwa zoezi la kuwaingiza wanachama wapya lisimamishwe mpaka hapo mkutano kama huu utakapotoa maamuzi mwengine
TDG4-9: Tarehe ya mkutano ujao
Mkutano umeweka tarehe 15/5/2012 saa 4.00 asubuhi kuwa ndio tarehe na sa ya mkutano ujao utakaofanyika Arusha Hall
TDG4-10: Kufunga mkutano
Mkutano ulifungwa na mwenyekiti tarehe 12 Aprili 2012 saa 11 Jioni
Im esainiwa na:
_______________________________________________ | _______________________________________________ | |
Mwenyekiti | Katibu |