Jifunze namna bora ya kuandika mpango mkakati kwa ajili ya kikundi, ofisi au shirika lako.
Ili uweze Kuandika Mpango Mkakati, kwanza tujue mpango mkakati ni nini na unatakiwa wakati gani?
Mpango mkakati ni taarifa iliyoandikwa kwa lugha rahisi kueleweka yenye kuonyesha dira ya taasisi husika na mambo gani yatawekwa kipaumbele katika kipindi cha miaka 3 hadi mitano ijayo ili kuweza kufikia dira tarajiwa. Taarifa ya mpango mkakati ni lazima pia ionyeshe rasilimali fedha, watu na vitu vitakavyotumika kufikia maono au dira
Wakati gani mpango mkakati unatakiwa
Ni pale tu taasisi inapotaka kufikia kwa ufanisi lengo fulani au pale taasisi husika haifanyi vizuri kwenye matumizi ya muda, fedha, watu na vitu na pia imebainika wazi kuwa malengo hayataweza kufikiwa. Hii inaweza kufahamika tu kama taasisi itaamua kujitadhmini. Ili kufaahamu zaidi ni wakati gani huu mpango unahitajika hebu turudi nyuma kwenye mwanzo wa kutumika neno mkakati wambao ndio msingi mkuu wa neno Mpango mkakati. Hili neno lilianza kutumika vitani, jeshi lilipozidiwa na maadui walirudi nyuma na kujiwekea mkakati wa kurudi vitani na kushinda vita
Hatua za kuandika mpango mkakati
Hatua ya kwanza
A: Uchambuzi yakinifu wa mahitaji
Watumiaji wakuu wa mpango mkakati ni taasisi husika na watu wake. Kama mshauri na mtaalam unatakiwa kufanya uchambuzi wa mahitaji ya msingi kuanzia wapi taasisi inataka iwe katika muda husika (yaani maono yao ni ipi), changanua changamoto zao zote na mbinu rahisi wanaweza kutumia ili kuzitatua. Changamoto (issues) ndizo zitakazotumika kutengeneza malengo na mikakati. Pia wadau wa mpango mkakati waeleze ni nidhamu na tunu (core values) zipi watazihatamia ili waweze kutekeleza huo mkakati
Uwahusishe kadri iwezekanavyo wahusika ili iwe rahisi pia wakati wa utekelezaji wa mpango mkakati.
Kumbuka madhumuni hayatakiwi yazidi saba, inashauriwa hasa hasa ziwe 5 au namba karibu na hapo yaani 5+-2 (isizidi 7 wala isipungue 3)
Namna ya kufanya uchambuzi
- Kutumia madodoso ili kupata maoni ya wadau wa taasisi
- Vikao vya faragha na viongozi / watu muhimu wanaoijua taasisi au wadau husika
- Mkutano na wadau wote
Hatua ya Pili
B: Ukusanyaji wa taarifa/takwimu na kazi katika vikundi
Kutengeneza Maono, Wito, Malengo mahsusi, tunu za taasisi, viashiria vya ufanisi, Tadhimini nk
Kazi hii itafanywa kupitia uwezehswaji na kazi za vikundi
Hatua ya Tatu
C: Kuandika Rasimu ya Mpango Mkakati
Kazi hii ili iende haraka inatakiwa kuandikwa na mtaalamu kwa kutumia taarifa zilizopatikana kutoka kwa wahusika wenyewe
Mfumo na mtiririko wa Mpango Mkakati ni kama ifuatavyo
- Muhtasari wa Mpango Mkakati
- Shukurani
- Utangulizi kwa kuweka historia fupi ya taasisi na muunganiko wake katika maono yake hapo chini
- Wasifu wa Taasisi (Institutional Profile
- Tamko la maono (Vision Statement)
- Tamko la utume (Mission statement)
- Tunu za msingi (Core Values)
- Uchambuzi wa nguvu na udhaifu wa kitaasis (SWOT Analysis)
- Malengo ya Kimkakati (Strategic Objectives)
- Changamoto za Kimkakati (Strategic Challenges) kwa kila lengo hapo juu na mbinu za kuzitatua
- Kuweka viasharia vinavyohakikishika ili kupima ufanisi (Objectively Verifiable Indicators) tumia LOGRAME hapa
- Mpango Kazi – Action Plan
- Bajeti ya Kutekeleza Mpango Mkakati – Budget Planning
- Ufuatiliaji na tathmini ya ufanisi – tumia jedwali
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |