Saladi ni mchanganyiko wa matunda mbalimbali au mbogamboga zinazoliwa bila kupika. Pia huitwa kachumbari ya matunda au mboga mboga.
Kuna aina tatu za saladi au kachumbari ambazo ni;
- Saladi ya matunda tu
- Saladi ya mbogamboga tu
- Saladi ya mchanganyiko wa matunda na mbogamboga
1. Saladi ya Matunda
Kama tulivyosema pale juu ni machanganyiko wa matunda mbalimbali. Unaweza kuandaa saladi hii kulingana na matamanio yako, uhitaji wa mlaji, bajeti yako au upatikananji wa matunda.
Mfano :
Vyombo vinavyohitajika kwa watu 4 -6:
- Bakuli au sahani safi
- Kisu
- Vijiko
- Sufuria
Vitu vinavyohitajika:
- Nanasi 1 kubwa
- Embe 2 makubwa
- Tikitimaji 1 dogo
- Papai 1 dogo
- Machungwa 2 madogo
- Ndizi 3 kubwa
- Kokomanga 1 dogo
- Matunda damu 3
- Zabibu mkungu 1
- Sukari vijiko 5
- Maji ya moto nusu jagi
- Pilipili manga vijiko 2 vidogo
- Mayonise (kama utahitaji au unapenda) vijiko 2 vidogo
Maandalizi kabla ya kuanza kuandaa saladi:
- Osha matunda yote kwa maji ya uvuguvu ili kuua vijidudu vya maradhi
- Yakaushe na yamenye na kuyaweka kwenye vyombo visafi (angalau vilivyosafishwa na maji ya uvuguvu na kukaushwa)
- Chemsha maji kisha changanya sukari na pilipilimanga (yaache yapowe)
Hatua za Kutengeneza Saladi Yenyewe :
- Kata matunda katika vipisi vidogo vidogo
- Weka kwenye bakuli na kisha changanya
- Chukua mchanganyiko wako wa maji, sukari na pilipilimanga kisha changanya kwenye matunda
- Changanya mchanganyiko wako kisha tayarisha kwa ajili ya kula
Kumb: unaweza kupamba matunda kwa namna yoyote ili yamvutie mlaji
Mfano:
2. Saladi ya Mbogamboga
Saladi hii ni mchanganyiko wa mbogamboga mbalimbali ambazo unaweza kupika na zingine si zakupikwa. Hivyo kuna aina mbili za saladi ya mbogamboga nazo ni;
- Saladi iliyopikwa
- saladi isiyopikwa
Saladi iliyopikwa
Saladi hii inahusika na mbogamboga amboazo haziwezi kuliwa bila kupikwa.
Mfano:
Mahitaji kwa watu 4-5:
- kabeji 1 kubwa
- lettuce kifungu kimoja
- karroti 3 kubwa
- pilpilimanga 2 vidogo
- tango 2 kubwa
- hoho 2 ndogo
- mayonnaise ½ kijiko
- kitunguu 1 kikubwa
- limao au vinegar vijiko 2 vidogo
Maandalizi kabla ya kuanza kuandaa saladi:
- osha kila mboga
- menya maganda
- katakata kabeji, lettuce, karoti, na hoho.
Hatua za kutengeneza saladi yenyewe :
- pasha pamoja kabeji, lettuce, karoti, hoho, na uweke chumvi.(dakika 5 tu)
- Wakao huo katakata tango na kitunguu kisha changanya na
- Chukua mayonise changanya na pilpilmanga
- Epua zile kabeji kisha acha ipoe
- Anza kuchanganya kabeji na mchanganyiko wa tango na kitunguu kisha weka limao
- Kisha weka mayonnaise yenye pilipilimanga
- Kisha kata tango linguine kwa ajili ya kunakshi
Mfano:
Saladi ambayo haijapikwa
Saladi hii inatengenezwa na mboga mboga ambazo zinaliwa bila kupikwa
Mfano:
Mahitaji kwa watu 4-5 :
- Kitunguu 2 vikubwa
- Nyanya 3 kawaida
- Tango 1kubwa
- Karoti 2 kubwa
- Chumvi vijiko2 vidogo
- Pilipilimanga 2 vijiko kidogo
- Limao 1 dogo
- Figisi 2 kubwa
Maandalizi kabla ya kutengeneza saladi:
- Osha mboga zote
- Menya maganda
Hatua za kutengeneza saladi yenyewe :
- Katakata nyanya, tango, karoti, figisi, kisha changanya
- Kamua limao kisha changanya na pilipilimanga na chumvi
- Changanya na mchanyiko wa limao
- Changanya mboga pamoja na mchanganyiko wa limao
- Weka nakshi
3. Saladi ya mchanganyiko
Saladi hii ni mchanganyiko wa saladi ya mbogamboga na saladi ya matunda . salkadi ndio kuu kuliko zote kwa sababu ina ladha nzuri pia ina ongeza virutubisho vingi zaidi kuliko hiza nyingine
Mfano :
Mahitaji kwa watu 4-5 :
- Zabibu mkungu 1
- Tango 1 kubwa
- Karoti 2 kubwa
- Figisi 1 kubwa
- Pilipilimanga kijiko 1 kidogo
- Juisi ya machungwa ½ kikombe
- Machungwa 2 makubwa
- Maembe 2 makubwa
- Ndizi 2 kubwa
- Kokomanga 1 kubwa
- Peasi 1 kubwa
Maandalizi kabla ya kutengeneza saladi:
- Osha matunda na mboga kwa maji masafi
- Menya maganda
Hatua za kutengeneza saladi yenyewe :
- Katakata mboga na matunda
- Changanya vyote
- Weka pilipilimanga kisha changanya
- Malizia na juisi ya machungwa kisha changanya
- Unaweza kunakshi
Asante Na karibu
Mwisho (End):
Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi
If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.
Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:
English Form |
Fomu ya Kiswahili |