Register

18 + seventeen =

A password will be e-mailed to you.

Baada ya kumalizia usajili wako wa kampuni au jina la biashara kwenye website ya BRELA utataka sasa kufanya malipo ya ada husika. BRELA inawapa wateja wake njia tatu (3) za kufanya malipo kama ifuatavyo:

Njia za kulipia Huduma:

 1. Kuweka Benki: Kwa njia ya kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
  Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
 3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha:  Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako

Malipo kupitia MPESA ya Vodacom Tanzania

 1. Kwenye eneo la kupiga simu andika *150*00# na ubonyeze kitufe cha kupiga simu
 2. Chagua # 4 – Lipa kwa MPESA
 3. Chagua # 4- Namba ya kampuni yenye tarakimu sita (6)
 4. Ingiza namba ya kampuni
 5. Ingiza kumbukumbu ya malipo (weka control namba kama ilivyoonyeshwa kwenye PO ya BRELA
 6. Ingiza PIN namba ya MPESA (Namba yako ya siri ya kuingilia kwenye akaunti yako ya MPESA)
 7. Ingiza moja (1) kukubali muamala
 8. Utatumiwa ujumbe mfupi kama huu

Malipo yamepokelewa kwenye Business Registration and Licensing Agency

Ankara Na: xxxxxxxxxxxx

Kiasi: xxxxxxxxx TZS

Risiti Na:  xxxxxxxxxxx

Tarehe: 20xx-xx-xxTxx:xx:xx

Kupitia: xxxxxxxxxxxxxxxx

x = namba

Baada ya malipo rudi kwenye akaunti yako ya BRELA na huisha (refresh) na utakutana na ujumbe wa rangi ya kijani ukisema malipo yamekamilika na maombi yametumwa BRELA kwa uhakiki

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

__________________________________________________
We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


Leave a Reply

city, country
mji, nchi