Ripoti ya fedha kwa taasisi ndogo ina sehemu kuu tatu
1. Mpango wa matumizi kwa muda uliopita
- Taja kwa mstari mmoja umepanga kutumia pesa kwenye nini na kwa kiasi gani
2. Ripoti yenyewe ya matumizi kwa muda uliopita
2.1. Matumizi yaliyopangwa
Weka jedwali linaloelezea mtiririko wa mapato na matumizi kwa kufuta jedwali hili
Na. | Tarehe | Maelezo ya mapato au matumizi | Kiasi | Baki | Bajeti | Maelezo | |
Mapato | Matumizi | ||||||
Mwanzo wa muda | Kiasi kilicholetwa kutoka muda uliopita | 2,654,000.00 | 2,654,000.00 | 2,654,000.00 | 100% | ||
1 | 04-Jan-18 | Usafiri | 245,000.00 | 2,409,000.00 | 200,000.00 | -23% | |
2 | 05-Jan-18 | Umeme | 45,000.00 | 2,364,000.00 | 43,000.00 | -5% | |
3 | 06-Jan-18 | (Maelezo ya pesa iliyoingia) | 350,000.00 | – | 2,714,000.00 | 350,000.00 | 100% |
4 | 07-Jan-18 | Usafi | 120,000.00 | 2,594,000.00 | 140,000.00 | 14% | |
31-Jan-18 | Jumla | 3,004,000.00 | 410,000.00 | 5,188,000.00 | 3,387,000.00 | 88% | |
31-Jan-18 | Kwenda muda ujao | 5,188,000.00 |
2.2. Ripoti ya tofauti ya matumizi
Na. | Maelezo ya tofauti kubwa ya matumizi |
1 | Bei za usafiri ziliongezeka zaidi ya ilivyobajetiwa |
4 | Tuliweza kuwashawishi kampuni za usafi watupe punguzo la gharama za usafi |
2.3. Matumizi yasiyopangwa na sababu zake
Matumizi yasiyopangwa ni aina ya matumzi ambayo haitakiwi kabisa katika ulimwengu wa matumizi ya fedha. Lakini kama imetokea kwa bahati mbaya ni lazima iripotiwe kwa heshima zote za fedha. Kwa maelezo ya sentensi weka kiasi ulichotumia, sababu za matumizi na akaunti ya matumizi.taasisi nyingi huwa wanaweka kwenye bajeti matumizi ya dharura au ya mkuu wa ofisi kwa ma ni meneja anawekewa matumizi ya jumla yaani general expenditure.
3. Changamoto zilizojitokeza na utatuzi wake
- Elezea changamoto ulizokutana nazo katika muda wa ripoti husika
- Ni vyema pia ukaelezea na njia au hatua mlizochukua kukabiliana na hizo changamoto zisiadhiri bajeti na shughuli za kawaida
4. Mpango wa matumizi kwa muda ujao
Toa picha ndogo ya mwonekano wa mapato na matumizi ya muda ujao
5. Hitimisho
Hitimisha kwa maneno yako kuhusu ripoti, maoni ya mambo unayotaka uongozi ufanye ili mambo yaende vizuri kama ilivyopangwa kwenye bajeti
6. Viambatanisho
Ambatanisha vielelezo vyovyote vitakavyoipa nguvu na maana na heshima ripoti yako
Mfano
- Nakala ya bajeti kwa muda uliopita na ujao
- Nakala ya wadai na wadaiwa wa taasisi ndani nan je yaani wafanyakazi na wasio wafanyakazi bila kutaja majina yao
- Nakala ya mikataba kama mojawapo ya mapato au matumizi ilijumuisha kuingia mikataba
- Nakala ya risiti kwa matumizi makubwa sawasawa na sera ya utawala na fedha kwenye taasisi yako, mfano manunuzi ya machine, kodi ya pango nk. Risiti zile za petty cash usiweke hapa
Taarifa:
Tunaweza kutoa huduma hii kwa gharama kidogo, huduma yenyewe yaweza kuwa ni ushauri, mafunzo au kufanya kazi husika. Tunatoa pia huduma ya masafa kupitia chat, email, mitandao ya kijamii nk
We offer services at substantial low cost. The service are consultation, training and doing personally the actual work. We also offer services remotely through chat, email, social media interfaces etc
English Form | Fomu ya Kiswahili |
[…] ya fedha […]