shule ya sekondari

Jinsi ya Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari

Hatua muhimu za kufuata ili kuanzisha shule imeelezewa vizuri katika ukurasa wa Hatua 5 za kuanzisha na kusajili shule. Katika ukurasa huu tutaelezea kwa ufupi sana mambo muhimu zikiwepo za kisheria ambazo utatakiwa kuzifuata ili shule iweze kuanza kufanya kazi na kukua.

Mambo 10 muhimu ya kuzingatia katika kuanzisha shule

  1. Matakwa ya kisheria kwenye umiliki wa shule. Mmiliki anaweza kuwa ni 1) mtu binafsi, 2) NGO au 3) kampuni? 4) Jumuiya, 5) NK.
  2. Matakwa ya kisheria kwa mamlaka ya udhibiti kwa suala la shule ni Kamishina wa Elimu wizarani – Pata kibali cha kuendesha shule kutoka kamishina wa elimu – andika barua ya kuomba kuanzisha shuel kwa kamisha wa elimu makao makuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia halafu kopi iende kwa mkaguzi mkuu wa elimu wa kand ambako shule itaanzishwa- Maelekezo menmgine utapewa huko.
  3. Kumiliki ardhi kwa kiwango cha chini cha wizara, afisa elimu wa mkoa au wilaya anaweza kukusaidia kwenye hili,. Au kuwa na mkataba wa kukodisha majengo yanayokidhi matakwa ya wizara kwa ajili ya shule.
  4. Matakwa ya kisheria kwenye ulipaji wa kodi – TRA Kama unatakiwa kulipa kodi ni lazima uripoti TRA upate TIN na ukadiriwe kiasi cha kulipa – Yaani Provisional Tax.
  5. Matakwa ya kisheria kwenye masuala ya afya – Kuchukua cheti cha afya kinachotolewa na Bwana Afya ambayo inadhibitisha kuwa eneo la shule linafaa kwa matumizi ya shule na kwamba haitahatarisha usalama wa kiafya ya wanafunzi na wafanyakazi wote
  6. Matakwa ya kisheria kwenye leseni ya eneo la ofisi yaani leseni ya Halmashauri husika- Pata leseni ya kukuhalalishia kufanya kazi pale ulipo, watoa leseni ni halmashauri husika.
  7. Matakwa ya kisheria kwenye Majengo – Mhandisi wa wilaya au Jiji, manispaa – Mhandisi wa manispaa au halmashauri wana rasimu ya michoro ambayo unatakiwa kufuata, hata BOQ wanaweza kukupa. Unaweza kutengeneza ramani yako na BOQ lakini ni lazima mhandisi wa Manispaa/halmashauri wakishirikiana na ofisi ya afisa elimu husika katika kuhakiki kama michoro inakidhi matakwa ya serikali. Mojawapo ya majengo yanayotakiwa ni Madarasa, ofisi za waalimu, jengo la utawala, bwalo, vyoo, maabara ya kompyuta na maabara zingine, miundo mbinu ya maji, miundo mbinu ya sehemu ya michezo nk.
  8. Majengo yaliyo na vifaa muhimu mfano, 1) Madarasa yakiwa na ubao, viti na ofisi ndogo ya mwalimu, Maabara yakiwa na vifaa vyake, ofisi za waalimu na samani zake, nk.
  9. Uongozi wa shule, nafasi hizi ni muhimu ili kupata usajili, 1) Meneja wa shule, Waalimu wenye sifa,
  10. Mtaji wa kuanzisha na kuendesha shule angalau kwa mwaka mmoja kwa ajili ya kulipa kodi, leseni, mishahara na kulipia gharama za kiutawala NK.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi