‘CORONA’ ni ugonjwa wa virusi (COVID-19) unaoambukizwa kwa kuingiwa na majimaji ya yatokayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye ugonjwa huu anapokohoa au kupiga chafya. Njia nyingine ya maambukizi ni kugusa majimaji yanayotoka puani (kamasi), kugusa vitambaa a nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huu. Ugonjwa huu unaambukizwa pia kwa kugusa popote ambapo mtu mwenye maambukizi amegusa kama vitasa vya milango, meza, makaratasi, vyombo vya chakula, vifaa vya ofisini, milango ya magari, helmet za pikipiki, usukani wa magari, meli, vitufe vyote vya kompyuta, simu, mitambo nk

DALILI ZA HOMA YA CORONA

 1. Homa kali
 2. Mafua
 3. Kikohozi
 4. Kubanwa mbavu na kupumua kwa shida
 5. Mwili kuchoka
 6. Maumivu ya misuli
 7. Vidonda kooni
 8. Kuumwa kichwa

JINSI YA KUJIKINGA NA HOMA YA VIRUSI VYA CORONA

 1. Epuka safari zisizo za lazima wakati huu wa mlipuko na inapolazimu kusafiri pata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza safari. Safari ni pamoja na kutembelea jirani, jamaa na marafiki wa hapo jirani na wewe au mbali na unakoishi.
 2. Unapoongea na mtu uso kwa uso kaa mbali zaidi ya mita moja, mita pendekezwa ni mbili.
 3. Epuka kusalimiana na kushikana mikono, kukumbatiana au kubusiana
 4. Nawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kila kuifanya tukio la kushika vitu vilivyoshikwa na watu wengi
 5. Funika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono au nguo uliovaa sehemu ya mkono
 6. Epuka kugusa pua, mdomo na macho kwa mikono
 7. Toa taarifa kwenye kituo cha karibu yako cha huduma za afya uonapo mtu aliyetoka nje ya nchi au mwenye dalili za ugonjwa kwa kupiga namba 0800110124 au 0800110125