Usajili wa NGO-CBO na Gharama Zake

Taratibu za Kusajili NGO/CBO na Gharama Zake

1.0 TARATIBU ZA USAJILI

Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unaofanyika chini ya sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002 umegawanywa katika ngazi nne kama ifuatavyo:

1.1  Ngazi ya Wilaya

1.2  Ngazi ya Mkoa

1.3  Ngazi ya Taifa

1.4  Ngazi ya Kimataifa

Msajili wa Mashirika ya kiserikali amepewa mamlaka chini ya kifungu cha 22(1) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, ya mwaka 2002 kuteua maafisa wa umma katika wilaya au mkoa kwa ajili ya kuwezesha usajili katika ngazi husika. Katika mfumo uliopo sasa maafisa wa umma wanaotajwa katika sheria ni Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya na Mkoa ambao kwa namna nyingine huitwa wasajili wasaidizi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 12(1) cha sheria, maombi ya usajili yatawasilishwa na kikundi cha watu kwa Msajili kupitia fomu maalumu (NGO A Fomu Na. 1). Maneno “kikundi cha watu” yanahusisha kikundi cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Hata hivyo, kanuni ya 3 ya kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia tangazo la serikali Na. 8 inaweka sharti la kikundi kuwa na watu/wanachama wasiopungua watano.

Kulingana na Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya NGOs Na. 24/2002, Maombi ya usajili wa NGOs yanatakiwa kuwa na viambatanisho vifuatavyo:-

  1. Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali (Nakala 3 zilizojaladiwa – Bound).
  2. Maelezo binafsi (Wasifu) wa viongozi 3 (CV) na picha 2 kwa kila CV – (Mwenyekiti, Katibu na Mhazini, au wengineo kulingana na mahitaji ya Shirika)

Angalizo: kwa NGOs za Kimataifa – CV mbili ziwe za raia wa Tanzania.

  1. Muhtasari wa kikao cha kuanzishwa kwa Shirika ukiambatanishwa na majina na saini za wanachama waanzilishi.
  2. Fomu ya maombi ya usajili (NGO A Fomu No. 1) iliyojazwa na mwombaji/waombaji na kubandikwa ushuru wa stempu za shilingi 1,500/= au Dola za Kimarekani 2 kwa NGOs za Kimataifa.
  3. Barua ya Utambulisho kutoka kwa Msajili Msaidizi (Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa, Halmashauri /Manispaa/Wilaya).
  4. Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.

2.0    ADA ZA USAJILI

a) Ngazi ya Wilaya Shs  80,000/=
b) Ngazi ya Mkoa Shs 100,000/=
c) Ngazi ya Taifa Shs 115,000/=
d) Ngazi ya Kimataifa Dola za Kimarekani 350

Maombi yatumwe kwa;

Msajili wa NGOs,

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,

8 Barabara ya Kivukoni

S.L.P 3448

11486 DAR ES SALAAM.

Simu 213526/2137679/2123146

Tovuti -http//www.tnnc.go.tz

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi