Mafunzo(Elimu) ya Masoko Kwa Wafanyabiashara Wadogo

Mafunzo(Elimu) ya Masoko Kwa Wafanyabiashara Wadogo

Yafuatayo ni dondoo fupi ya namna ya kufundisha Mafunzo (elimu) ya Masoko Kwa Wafanyabiashara au wajasiriamali wadogo wadogo. Imeanza na kutathmini hali ya sasa, dhana ya masoko, taarifa za wateja, hatua za kuchukua ili kutekeleza zoezi la kutafuta masoko, kalenda ya kufanya masoko, njia za kuwafikia walengwa, kutekeleza utafutwaji wa masoko na mwisho ni kutathmini kama zoezi linaleta matokeo tarajiwa au la kupitia  ripoti na taarifa mbalimbali .

A) Hali ya sasa

Majadiliano: Mwezeshaji na wawezeshwaji

 1. Wanauza wapi, nini, lini, bei gani, nk?
 2. Mafanikio mpaka sasa – taja na muda wa mafanikio
 3. Hatua zilizochukuliwa ili kuendeleza mafanikio hayo
 4. Changamoto – taja na muda wa changamoto
 5. Hatua zilizochukuliwa ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto hizo
 6. Maoni

B) Dhana ya masoko

  1. Vichwa (Leads) (Hawa ni wale watu wote wanaofuatilia ili kuijua biashara yako zaidi. Bado hawajaanza kununua kutoka kwako)
  2. Wateja wapya(Hawa ni wale watu wote walioanza kununua kutoka kwako kwa mara ya kwanza)
  3. Wateja wa kudumu (Hawa ni wale watu wote wanaonuanua kutoka kwako mara kwa mara)
  4. Huduma kwa wateja (Hii ni huduma nzuri kwa wateja ili warudi tena kununua kutoka kwako- Huduma yaweza kuwa ni msaada wanaposhindwa kutumia bidhaa uliowauzia, maswali waliyonayo juu ya huduma na bidhaa zako, salamu na au kumtembelea mteaja ili ujue anaendeleaje na maelekezo au mawasiliano yote kati yako na mteja)

Vichwa – Leads

Kujau vizuri hii dhana ya masoko ndio chachu ya wewe kujua ukweli wa masoko na naman gani utaifanya kwa ufanisi mkubwa

Unapoitangaza biashara yako unavutia hisia za watu wengi kutaka kujua zaidi juu ya biashara yako

Wengine watakutembelea ili kuuliza maswali, wengine watakupigia simu kwa lengo hilo hilo la kujua zaidi, wengine watakuandikia email, whatsapp au wengine watakutembelea kabisa kwenye mitandao ya kijamii kama Youtube, Facebook, Twitter, Instagram, Linkedin, Google nk kama unazo hizo huduma.

Ikitokea hivyo hao ndio tunawaita vichwa au leads kwa kimombo

Wateja

Wateja ni wale watu wote wanaonunua kutoka kwako. Hawa wanaweza kuwa ni wateja wapya au wateja wa kudumu

Wateja wapya kama wameanza kununua kwa mara ya kwanza, wakirudi rudi kununua wanabadilika na kuitwa wateja wa kudumu

Huduma kwa Wateja

Huduma kwa wateja ni dhana kubwa kuliko maana yake ya halisi

Haya ni mawasiliano kati ya mtoa huduma na mteja

Mawasiliano yanaweza kuwa yafuatayo

 1. Kumpa mteja taarifa za bidhaa mpya
 2. Taarifa za ofa na punguzo la bei
 3. Taarifa za kupanda kwa bei
 4. Taarifa za mabadiliko ya utoaji huduma au sera za mahusiano
 5. Kujibu maswali na kero au malalamiko ya wateja
 6. Kuwasalimia wateja kwenye siku maalumu kama za sikukuu, maadhimiso ya biashara yako, siku maalumu duniani, birthday ya mteja, birthday ya mtoa huduma nk
 7. Kumsalimia mteja na kujua kama anaendelea vizuri kwa maisha yake, au matumizi ya bidhaa au huduma uliyompa nk
 8. kumtembelea mteja kwake kwa lengo hilo hilo hapo juu
 9. kufanya seminar, kongamano, bonanza, sherehe maalumu ili kuongeza ukaribu wa mahusiano
 10. Kuendehsa tovuti, au mitandao ya kijamii kama Whatsapp, Youtube, Facebook, Twitter, Instagram, Linkedin, Google nk.

Mambo muhimu ya kukumbuka

 1. Biashara inayokua ina sifa hizi = Ina wateja wapya na wa kudumu wanaoongezeka
 2. Biashara inayodumaa ina sifa hizi = Inawateja wapya tu wanaoongezeka na wakudumu wanaopungua au ina wateja wa kudumu wanaoongezeka tu na wateja wapya wanaopungua
 3. Biashara inayokufa ina sifa hizi = Ina wateja wapya wanaopungua na wateja wa kudumu wanaopungua pia

C) Taarifa za wateja (customer’s database)

Taarifa zenyewe ni kama hizi hapa chini

 1. Jina la mteja                
 2. Simu   Email                
 3. Eneo analoishi             
 4. Shughuli anazofanya  
 5. Maoni

Unaweza weka kwenye jedwali kama hapa chini

No. Jina la mteja Simu Email Eneo analoishi Shughuli anazofanya Maoni

D) Hatua za kufuata katika kutekeleza utafutaji wa masoko

 • Kuchambua wateja wako kwa maana ya matakwa na mahitaji yao, uwezo wao wa kununua, miiko yao, wako wapi, wangapi, umri, dini, jinsia nk
 • Kwa biashara kubwa unaweza kumuajiri mtaalamu wa kukufanyia na kwa biashara ndogo unaweza fanya mwenyewe kwa kukisia ili iwe karibu na ukweli. Taarifa zingine unaweza kwenda kuzichukua kwenye serikali ya kitongoji, kijiji, mtaa au Kata

E) Kalenda-Mpango wa kufanya masoko

Tarehe – Shughuli, Kusudi – Mahitaji – Bajeti Mhusika-Maoni

Weka kalenda yako kimkakati, unaweza omba ushauri kwa anayejua kama hujui naman ya kuanza

Tarehe Shughuli Kusudi Mahitaji Bajeti Mhusika Maoni

F) Njia kuu za kuwafikia walengwa

 1. Radio
 2. TV
 3. Magazeti
 4. Mikutano/kongamano/warsha/semina
 5. Tovuti (website)
 6. Gari la matangazo
 7. Mabango
 8. Vipeperushi/vitabu/majarida/Makala/Kadi nk
 9. Kutembelea ofisini/nyumbani

Kila njia hapo ina uzuri na ubaya wake, chagua njia yenye kuendana na biashara yako, wateja wako nk

G) Hatua ya Utekelezaji

 1. Weka ratiba ya kufanya kimkakati –  i.    Mfano: utaanza wapi na utaishia wapi?  ii.    Utaanza na njia gani?
 2. Anza na majaribio
 3. Endelea na njia bora

H) Tathmini ya Zoezi Nzima

 1. Je zoezi limefanikiwa kwa kiwango gani (Facts and Figures)
 2. Nini ilikuwa siri ya mafanikio hayo
 3. Je ni maeneo gani hayakufanya vizuri
 4. Nini ilikuwa changamoto ya kutofanya vizuri
 5. Mpango mkakati wa maboresho na kuanza tena

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi