Register

three + thirteen =

A password will be e-mailed to you.

Ukurasa huu utakuonyesha namna bora ya kugundua, kuendeleza na kutengeneza pesa kutokana na kipaji ulicho nacho.

USHAURI KWA VIJANA

Je wewe unacho kitu gani tofauti na wenzako katika mji wako?
Je ni nguvu zako?
Sauti yako?
Ubunifu stadi?
Ucheshi?
Usanii?
Uongeaji?
Ushawishi?
Uhamasishaji?
Mchezaji?
Uigizaji?
Uimbaji?
Upigaji wa vyombo vya muziki?
Utumiaji wa vyombo maalumu
Kutengeneza programu za computer/simu?
Ujenzi?
Ushonaji?
Ufundishaji?
Uongozi?
Mgunduzi?
Mtaalamu wa lugha?
Mpiga picha maridadi?
Mchekeshaji?
Na zaidi na zaidi?

Kwa ngazi yeyote ya elimu yako
Sikiliza huu ushauri

Je unajua kwamba unacho hicho kipaji?
Kama ndio
Jiulize hicho kipaji ambao ni tofauti na wengine kimekusaidia nini tangu ujue kwamba unacho?
Kama sio fanya yafuatayo:
Fanya jambo ambalo hata usipolipwa utalifurahia kul;ifanya kwa ustadi, ubunifu na mafanikio
Unaweza pia rudi nyuma utotoni na kujaribu kuscan zile michezo uliyokuwa unayapendelea kufanya na kufurahia. Je inaangukia kwenye secta ipi?
Ualimu, uhandisi, sanaa, utafiti? nk
Jaribu kuyafanya yanayoendana na huo ugunduzi kila mara. Baada ya muda fulani utajikuta ukipenda sana kufanya mambo machache kuliko zile za mwanzo. Sasa unaelekea kwenye taaluma yako.
Ongeza bidii kwa kuyafanya kwa ubunifu na ari zaidi ukijizoeza kwamba motisha yake iwe ni kwenye kuifanya kwa ufanisi na sio kulipwa

Kumbuka malipo humfuata mbunifu, mchapa kazi na mpenda kazi

Ukisha jitambua kuwa sasa wewe ni wa secta ipi na uko tofauti na wenzako katika hilo eneo, fanya yafuatayo?

Tafuta maeneo ambayo unaweza jitolea kufanya kazi bure wakati wako wa ziada

Ukijitolea itasaidia mambo matatu

  1. Kukubalika
  2. Kuibua kipaji chako
  3. Kupata fursa ya kutumia vifaa muhimu za ofisi husika zitakazosaidia kipaji chako kukua zaidi na kwa haraka

Wakati unajitolewa, utajionyesha pia kwa waajiri wengi na hivyo watakuona na kuchukuliwa – Yaani umepata kazi

Kama unataka ushauri zaidi andika wasifu wako
Ambatanisha na barua yako yenye kujieleza zaidi, elezea kipaji chako kwa undani kwenda kwa

info[@]kivuyo.com au info[@]tanzaniaconsultants.com (ndoa mabano)

English Form

Fomu ya Kiswahili


About The Author

Lemburis Kivuyo is a Busi­ness, IT and Com­mu­nity Related Project Consultant. Specialized in Business Establishment, Leadership training, Online Marketing, Small groups and teams leadership and management, Curriculum Development, Constitution development and much more.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.

1 × one =

PO Box 1999, city, country
SLP 1999, mji, nchi