Jinsi Ya Kuandika Andiko La Mradi

Jinsi Ya Kuandika Andiko La Mradi

Warsha ya andiko la mradiUtangulizi:

Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa kitaasisi na kifedha

 1. Mradi huo unaitwaje? Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
 2. Historia ya tatizo: Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo lilianza nkwa nani?
 3. Kwanini tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki? Je, mradi ni suluhisho halisi na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
 4. Mpango wa utekelezaji: Unaweza kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje katika jamii hii.
 5. Usimamizi wa mradi: Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?
 6. Malengo au Lengo kuu la mradi ninini? Madhumuni yake mengine ni yapi? Shughuli za mradi na majukumu madogomadogo ninini? Ambayo lazima yapangwe kimantiki na kwa matarajio yenye kufikia lengo.
 7. Uchambuzi wa wadau wa mradi: Ni wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu, mchango wa wadau hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu ?
 8. Masuala mtambuka: Kuna uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala la mazingira linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na magonjwa yasiyotibika yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa mradi huu?
 9. Ufuatiliaji na tathmini ya mradi: Umepanga kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za mradi huu? Uendelevu wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu kwa namna gani?
 10. Uendelevu wa mradi: Je kuna mipango madhubuti yatakayowezesha mradi kuendelea kuwepo hata baada ya ufadhili kuisha?
 11. Bajeti ya mradi: Ainisha ghrama za ununuzi wa vitu, malipo ya mishahara na gharama zingine zitakazohitajika ili kuendesha mradi

NB: Maswali haya yakijibiwa vizuri kwa mtiririko sahihi huitwa andiko la mradi na ifuatayo ndio mpangilio wa jumla ambao wahisani wengi wameupenda katika kuandika andiko la mradi.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Wasiliana nasi kupitia:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more
English Form

Fomu ya Kiswahili


Share On
city, country
mji, nchi