Hatua 7 za Kuwa Mjasiriamali-J7

Hatua Saba (7) Muhimu Ili Kuwa Mjasiriamali – J7

Ujasiriamali ni neno la kiswahili linalotokana na maneno mawili yafuatayo

 1. Ujasiri
 2. Wa mali

Hii ina maana ya mtu mwenye ujasiri wa kuwekeza mali alizonazo ili apate faida

Hatua 7 muhimu ili kuwa mjasiriamali kamili (J7)

 1. Jitoe bila woga na kuwekeza ulicho nacho,
 2. Jipange (mpango mkakati)
 3. Jipime Ili kujua uwezo na madhaifu yako
 4. Jiwezeshe kwa kupata mafunzo
 5. Jihadhari ili usitumbukie kwenye hatari
 6. Jitadhmini, jikosoe kwa kujitathmini
 7. Jipange upya kwa kufanya maboresho

1. Jitoe Bila Woga na Kuwekeza Ulicho Nacho

Maamuzi magumu yanatakiwa unapotaka kuwa mjasiriamali. mke, mume, wazazi, wajomba ndugu, marafiki, wakuu wa ukoo wako na hata mazingira yako yanaweza kukataa au kuwa pingamizi kubwa ili usifanye shughuli za kijasiriamali.

Kwa mazingira haya ni rahisi kukata tamaa na kama hukuamua kutoka moyoni mwako fikra zako za kuwa mjasiriamali zitaishia hapo na hutakaa ufanye biashara.

Kuamua na kujitoa ni muhimu sana ili uweze kuendelea an maono yako yatakayokukomboa kiuchumi

Ili uweze kujenga himaya yako (ufalme wako) (your kingdom) wa utajiri unahitaji kufanya maamuzi yako peke yako wala sio ya hao waliotajwa hapo juu japo ushauri kutoka kwao ni ruksa na utakusaidia kufanya maamuzi bora zaidi.

Kujitoa unakusaidia wewe kuhesabu gharama ya hatari zitakazokuwepo mbele yako kwenye ujasiriamali wako. Utahitajika saa nyingine kuwekeza mali ya kipekee uliyonayo. kama vile nyumba, gari, kiinua mgongo nk.

Kama wewe ni mwoga hutadhubutu kuwekeza kajumba kako ka-pekee eti kwa sababu ya ujasiriamali.

Kama kweli ukiamua na kujitoa maisha yako yatabadilika sana kuanzia siku ile ya maamuzi magumu.

Safari ya ujasiriamali huwa na tabia ya kwenda juu au chini kama meli inayoyokabiliana na tufani baharini. Unashauriwa kutizama lengo na sio tufani ya bahari. Kama umeamua kutoka moyoni kuwekeza utafika tu kwenye lengo kuu.

Epuka kukopa ili uanzishe biashara, ni hatari sana. Kusanya vyazo vyako vya mitaji (mali binafsi) na uanzishe biashara

2. Jipange (Mpango Mkakati)

Weka maono ya biashara yako, unataka kufikia ngazi ipi kimafanikio. Je unataka kuwa na hoteli kubwa ya kitalii au kiwanda kikubwa cha kuuza nguo Tanzania au Afrika nzima?

Weka na kazi muhimu utakazozifanya ili kufikia maono husika. Unaweza weka malengo mahsusi kila baada ya miaka mitatu au mitano. Inashauriwa malengo hayo mahsusi yawe kati ya 3 na 5.

Jiwekee malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Malengo yagawanywe mpaka kwenye kazi za kila siku.

Jiwekee maadili na tunu za mafanikio. Bila hizi tunu na maadili huwezi kuyafikia malengo yako.

Jiwekee ratiba mbalimbali za kiutekelezaji bila kusahau kuweka kwenye ratiba shughuli muhimu.

3. Jipime Ili Kujua Uwezo na Madhaifu yako

Kiingereza wanaita SWOT Analysis

Jipime juu ya mambo makuu manne yaliyogawanyika kwenye makundi mawili

 1. Mazingira ya biashara ya ndani
 2. Mazingira ya biashara ya nje

AU

 1. Mazingira wezeshi
 2. Mazingira hatarishi

Haya makundi mawili nayo yamegawanyika katika

Mazingira ya ndani ni

 1. Uwezo wako kibiashara
 2. Udhaifu wako kibiashara

Mazingira ya nje ni

 1. Fursa zilizopo ili kunufaisha biashara yako
 2. Hatari zilizopo ili kuua biashara yako

Mazingira wezeshi ni kama ifuatavyo

 1. Fursa zilizopo ili kunufaisha biashara yako
 2. Uwezo wako kibiashara

Mazingira hatarishi ni kama ifuatavyo

 1. Hatari zilizopo ili kuua biashara yako
 2. Udhaifu wako kibiashara unaoweza kuzorotesha maenedleo ya biashara yako

4. Jiwezeshe kwa Kupata Mafunzo

Jiwezeshe ni hatua inayojibu matokeo ya hatua ya kujipima ambayo imekuwezesha kugundua madhaifu yako na kuyapatia ufumbuzi kwa kujiwezesha ambazo mara nyingi ni mafunzo.

Udhaifu ni yale mambo ya kimaarifa usiyoyajua kiutendaji ili biashara yako isonge mbele.

Inaweza kuwa ni ujuzi wa kufuga samaki kama unataka kuanzisha mradi wa kufuga samaki nk.

5. Jihadhari ili Usitumbukie Kwenye Hatari

Katika hii hatua hakikisha kila uamuzi au tendo unalofanya halitakuingiza kwenye hatari kubwa usiyoweza kumudu bali inakuweka kwenye changamoto ambazo unazimudu. Kingereza wanaita (Moderate Risk).

 • Usijaribu kufanya biashara zenye hatari kubwa na ya uhakika.
 • Usijaribu kuingia ubia/ushirika na watu ambao unawajua ni hatyari kwa biashara zako.
 • Usijaribu kuingiza teknolojia kwenye biashara yako ambayo una uhakika kuwa sio rafiki.

6. Jitadhmini, jikosoe kwa Kujitathmini

Fanya  tathmini za mara kwa mara ili kujua kama unakwenda sawasawa na makusudio ya mwanzo.

Fanya tadhmini ndogo kila baada ya nusu mwaka, na tadhmini kubwa kila baada ya miaka mitatu.

7. Jipange Upya kwa Kufanya Maboresho

Matokeo ya tadhmini yatumike kama msingi wa kujipanga upya na kufanya maboresho makubwa yatakayoitoa biashara yako kutoka kwenye ngazi moja ya mafanikio kwenda ngazi ya juu zaidi ya mafanikio.

Tumia matokeo ya tadhmini zote mbili kujikosoa na kufanya maboresho yenye lengo la kujibu kasoro zilizoonekana kwenye ripoti ya tadhmini.

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi