Company Registration in Tanzania

Hatua na Jinsi ya Kusajili Kampuni au Biashara BRELA

TANGAZO KWA WASOMAJI WA UKURASA HUU

TangazoUtaratibu mpya wa kusajili kampuni kupitia mtandao umeanza rasmi tarehe 22 Machi 2018 na hapohapo BRELA kutangaza kutopokea tena nyaraka ngumu kuanzia tarehe 25 Machi 2018.

Kwa kuwajali watembeleaji na wafuasi wa tovuti ya KIVUYO>COM, nimeweka “Hatua 10 rahisi kabisa za kusajili kampuni yako kupitia mtandao wa BRELA“. Kama pamoja na taratibu hizo unaona bado unahitaji ushauri na au huduma kamili ya kusajili kampuni, wote mnakaribishwa kwa huduma nzuri, rahisi na ya haraka kwa gharama nafuu.

MAMBO MUHIMU YA KUJUA

  1. Ili kutumia tovuiti kwa kazi hii, jisajili kwanza ors.brela.go.tz halafu endelea na mahitaji yako ndani ya tovuti hiyo. Simu za brela zipo kwenye+ website kwa msaada zaidi
  2. Tamko la mwakilishi wa kampuni husika kufuata sheria zote za usajili ziko kwenye fomu na. 14b ambayo huapwa mbele ya hakimu.
  3. Maelezo ya wakurugenzi yako kwenye Consolidated Form ambayo hupakuliwa baada ya kujaza kwenye mfumo wa ORS maelezo yote muhimu ya usajili ambazo ni pamoja na maelezo ya wakurugenzi na wenye hisa (Zamani fomu hii iliitwa form nao. 14a)

Kwa maelezo zaidi kuhusu gharama za usajili bofya hapa

  1. Kusajili wa kampuni isiyo na hisa
  2. Kusajili wa kampuni ndogo ya chini hisa za Shs milioni 1
  3. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 1 hadi milioni 5
  4. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 5 hadi milioni 20
  5. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za Shs milioni 20 hadi milioni 50
  6. Kusajili wa kampuni ya kati hisa za zaidi ya Shs milioni 50

Gharama za usajili wa kampuni BRELA kwa ufupi ni

Hatua saba (7) muhimu za kufuata wakati wa kufanya usajili wa kampuni au jina la biashara

  1. Kulipia angalau 60% ya malipo yote, Kutuma taarifa zinazotakiwa (taarifa za kampuni, wenye hisa, wakurugenzi, katibu, hisa nk) – siku ya kwanza
  2. Utengenezaji wa nyaraka muhimu za usajili, utiaji saini na kupigwa muhuri wa mwanasheria – siku ya pili
  3. Kuanza mchakato wa maombi masafa na kupakia taarifa kwenye mtandao  – siku ya tatu
  4. Kufanya malipo ya usajili BRELA na kutuma maombi – siku ya tatu
  5. BRELA kuyafanyia kazi maombi kwa kuhakiki na kutoa mapendekezo kama yapo – siku ya nne, saa nyingine hapa huchukua siku nyingi zaidi hadi 3 au zaidi ya hapo
  6. Kuyafanyia kazi mapendekezo ya BRELA kama yapo kama hayapo ndio mwisho.  Kama marekebisho yapo, mchakato unarudi pale marekebisho yalipofanyikia. mfano kama marekebisho yamefanyikia hatua ya kwanza, mchakato wote unaanzia hapo nk – siku ya tano
  7. Kumalizia malipo 40% na kukabidhiwa vyeti na MemArt katika mfumo wa PDF

Kumb:

  1. Mchakato wote huchukua siku tano (5) kama BRELA hawakupendekeza marekebisho
  2. Siku za mchakato zinaweza kupungua kutoka siku tano (5) hadi siku tatu (3) kama taarifa zilizoletwa na mteja ni sahihi, zinajitosheleza na zimeletwa kwa kuwahi.
  3. Ikiwa BRELA watarudisha marekebisho ya jina au taarifa zingine, mzunguko wa mchakato utarudi na kuanzia pale marekebisho yamefanyika. mfano kama marekebisho ni ya jina basi mchakato utarudi na kuanzia kwenye hatua ya kwanza japo utekelezaji wake utaenda kwa haraka zaidi kwa sababu ni marekebisho tu. Kama marekebisho ni ya ujazaji wa fomu za BRELA tu basi mchakato utarudi kwenye hatua ya tatu nk.
  4. Mteja atalazimika kupendekeza majina ya kipekee (Unique names) matatu (3) kwa ajili ya usajili na jina la kwanza likibeba uzito zaidi ya jina la pili na kadhalika jina la pili likibeba uzito zaidi ya jina la tatu.
  5. Idadi ya marekebisho ya jina inayoruhusiwa kwa ada ile ile ni matatu tu, zaidi yahapo mteja atawajibika kulipa Shilingi elfu ishirini (Shs. 20,000) kwa kila jina linaloongezeka.

MZUNGUKO WA MCHAKATO WA KUSAJILI KAMPUNI BRELA

Maelezo zaidi ya namna ya kusajili biashara au kampuni BRELA

Mwisho (End):

Kama umependa makala hii weka maoni yako ya shukrani hapo chini au washirikishe marafiki zako wa kwenye Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter na kwenye email au mitandao mingine ya kijamii. Wasiliana nasi kama unataka kuweka kwenye blogu au website yako kwa maelekezo zaidi

If you found this article helpful please leave the comment below or share to your friends in Facebook, Instagram, Linkedin, Whatsapp, Twitter and in email or other social media. Contact us if you plan to list in your blog or website for further instructions.

Tutembelee kwenye mitandao ya kijamii hapa chini:

We offer but not limited to the following:
Business Office Documents Development, Company Registration, Business Plan Development, Curricula Development for colleges, Office Digitization Consultancy, Online Presence and Marketing Consultancy, Leadership and Management Consultancy, Constitution Development  and much more

English Form

Fomu ya Kiswahili


city, country
mji, nchi